Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Profesa Aldin Mutembei amililia Kezilahabi, aeleza alichokiacha

Profesa Aldin Mutembei kulia akiwa na Profesa Kezilahabi ujerumani enzi za uhai wake


Profesa Mutembei, mtaalamu wa fasihi kutoka katika taasisi ya taaluma za kiswahili Chuo kikuu cha Dar es salaam, ambaye amewahi kushirikiana na Profesa Kezilahab mambo kadhaa pamoja na kusoma kazi zake za kifasihi, katika mtandao wake wa kijamii aliandika yafuatako baada ya kifo cha mwandishi, mtafiti, Mwalimu na mtaalamu wa fasihi ya kiafrika Profesa Kezilahabi kuaga dunia katika alfajiri ya Jana January 9/2020

  "Mungu kamchukua Kezilahabi: 
Katuachia maandishi yake. 
Kachukua ucheshi na mzaha wake ,
Katuachia fumbo la kimya chake. 
Amechukua nguzo ya uthubutu katika ushairi 
katuachia mzozo wa vina na mizani. 

Kaondoka Kezi kaiacha Dar es Salaam anakwenda kupumzika Namagondo. 
Atalazwa katika eneo dogo ardhini alilolipenda.
Katika kona ndogo itakayoshikilia mwili wenye fikra kubwa.
Alipoleta “Kaptula la Marxi” hakutuachia fundi mshonaji, 
na sasa Kaptula hatujui kama linapwaya au limekaa sawa. 
Nyie, nani anavaa kaptula siku hizi?
Suruali zenyewe wanavaa “kata K”
Na siku hizi vijana wanashona nguzo za kubana, 
ukivaa kubwa ni mojawapo ya kigezo cha wakati. 

Lakini Kezilahabi, alihoji sana kuhusu wakati. 
Ni wakati gani atakaporejea kusuluhisha mgogoro huu wa kupwaya 
au kubana kwa nguzo zetu?
Kila wakati alipenda kuandika
Ataendelea kuandika
Nini? Mashitaka? Akimshtaki nani?
Akimshtaki kwa Nani?
Maana yule katekista aliyechukua jukumu la kusikiliza ungamo, 
alizuiwa na Padri Madevu kuendelea na kazi ambayo si ya kwake.
Ametuachia fikra
na kimya kikuu"

Post a Comment

0 Comments