Aliyekuwa mtaalamu, mwandishi na mtafiti wa lugha ya kiswahili, fasihi, na falsafa za kiafrika profesa Euprase Kezilahab amefariki dunia alfajiri ya leo January 9/2020. Baada yakupokea taarifa hizo mtandao huu Masshele Swahili umewasiliana na Prof Budzani Gabanamotse-Mogara ambaye ni Head, African Languages & Literature
Faculty of Humanities
University of Botswana
P/Bag 00703
Gaborone, Botswana Mkuu wa idara ya lugha na fasihi chuo kikuu cha Botswana ndaki ya Insia. Ambapo kwa masikitiko makubwa amesema
"Morning. It is true, I just received the sad news this morning" (ni kweli amefariki! Nimepokea taarifa hizi za uchungu asubuhi hii)
Ikumbukwe kuwa miaka miwili iliyopita mtandao huu ulifuatilia taarifa zake katika chuo hicho na kujibiwa kuwa Profesa Kezilahab hakuwepo Botswana bali Tanzania kutokana na maradhi
Historia Fupi
Anahitwa Profesa Euphrase KezilahabiKuzaliwa: Kazaliwa mwaka 1944, Namagondo, kijijini Ukerewe kisiwani (Lake Victoria)
Ni Profesa wa Kiswahili
Ni raia wa Tanzania
Elimu: BA and MA degrees (UDSM), MA, PhD University of Wisconsin, in Madison, USA (1982, 1985)
Alishawahi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kisha University of Botswana, Gaborone)
Vitabu alivyowahi kuandika: Mzingile (1991), Nagoma (1990), Karibu Ndani (1988), Cha Mnyonge Utakitapika Hadharani (1985), The Concept of the Hero in African Fiction (1983), Karibu ndani (1988), Gamba la Nyoka (1979), Waziri wa Maradhi (1978), Kaptula la Marx (1978, 1999) , Kichwamaji (1974), Kichomi (1974), Dunia Uwanja wa fujo (1975), Wasubiri Kifa (1976), Rosa Mistika (1971).
WADAU WAMLILIA
wadau mbalimbali wamemlilia nguli Huyu wa fasihi ya kiafrika katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Yarabi Mungu wa wema, mwanao ninakujia
Nalia ndani waama, kifo kiliotujia
Kumchukua daima, ghuli tulomwaminia
Lala pema kwao wema, Profesa Kezilahabi
Wengi tunalia sana, sisi tulomsikia
Huyu kweli muugwana, yeye alipoongea
Kinyongo kwake hakuna, lugha alipigania
Lala pema kwao wema, Profesa Kezilahabi
Hakukuwa mkosaji, mimi nilivyomjua
Safi livyokuwa maji, roho yake ilikua
Cha ukweli zuri taji, Kezilahabi chukua
Lala pema kwao wema , Profesa Kezilahabi
Tutakukosa kabisa, mwalimu pia mwandishi
Ila jinalo Profesa, mitimani litaishi
Pepo amekupa sasa, hilo hatuna ubishi
Lala pema kwao wema, Profesa Kezilahabi
Peponi ulikotoka, umerejea mwalimu
Nasi njiani hakika, tupo kwa nyingi hamumu
Peponi tuweze fika, twani ni letu jukumu
Lala pema kwao wema, Profesa, Kezilahabi
Kaditamati Karima, dua tunamuombea
Mjalie himahima, peponi akaingia
Ututulie mitima, yetu na ya familia
Lala pema kwao wema, Profesa Kezilahabi
Mtunzi - Wanjohi P Mugambi
Lakabu- Malenga Kitunguu Machoni
Thika Kenya 🇰🇪 "
![]() |
| Profesa Kezilahabi kushoto ukiwa na Profesa Aldin Mutembei Enzi za uhai wake |
Mtandao wa masshele Swahili unatoa pole kwa wote, hasa familia, wadau wa fasihi, lugha na falsafa za kiafrika, na wote kwa ujumla "KEZILAHABI UMEONDOKA LAKINI MAWAZO YAKO YATAISHI DAIMA"
msikilize profesa chini mwisho (footer)katika mtandao huu
Taarifa zaidi zitazidi kukujia mdau wetu


0 Comments