Hujambo ndugu msomaji, karibu tuangazie namna unavyoweza kutumia ujuzi wako wa lugha kujipatia kipato.
Lugha ni uchumi, na kuwa ujuzi wa lugha ulionao unaweza kukuinua kiuchumi. Hata hivyo ujuzi wa lugha mbalimbali kama vile kiswahili, kingereza, kijerumani, kisomali, kichina nk. Ni muhimu zaidi tunapozungumzia fursa zilizopo katika lugha. Zifuatazo ni njia unazoweza kufanya ili kujipatia kipato
1. Kuwa Mfasiri/ mtafsiri wa kujitegemea (free lence translator) Kupitia njia hii unaweza kufasiri kazi mbalimbali za watu binafsi au mashirika.
-Kuwa karibu na waandishi mbalimbali na waulize kama wangependa kazi zao fulani kutafsiriwa
-Omba kutafsiri baadhi ya machapisho maarufu na kuyauza upya, hapa itakupasa kutafuta riwaya au kazi yeyote inayovuma sana kisha kuitafsiri katika lugha uijuayo mfano unaweza kutafsiri kazi ya Chimamanda Ngozi ya Yellow Hibiscus kwa kiswahili na ukaiuza upya kumbuka kutafuta idhini
-Tafuta nafasi za kazi za kutafsiri mtandaoni, weka katika profail yako ya Linking, Facebook au twiter kuwa wewe ni mfasiri
-Anzisha kituo cha kutafsiri
2. Kuwa Mwongoza watalii, hii ni fursa nyingine inayotokana na ujuzi wa lugha ulionao
-Tafuta kituo cha utalii na uulize ni wageni wapi wanapenda kutembelea mfano wewe unajua kichina, na watalii wengi wanaotembelea mlima Kilimanjaro ni wachina basi tafuta fursa hapo
3. Anzisha darasa la watoto wanaotaka kujifunza lugha unayoijua (baby sitting a child who learng your native language)
Wazazi wengi hupenda watoto wao wajifunze lugha hivyo kama wewe ni mjuzi wa lugha Fulani kama vile kingereza unaweza kufungua kituo hiki mtaani Kwako.
4. Kuwa Mwalimu wa kufundisha lugha ya kigeni. Lugha unayoijua wewe kuna nchi hawaifahamu kabisa lakini wanahitaji kuifahamu tafuta fursa huko
-Tafuta wanafunzi mtandaoni, kwa kuanzisha program za kufundisha lugha au tovuti
-
5. Kutengeneza maudhui ya lugha uijuayo na kuyauza mtandaoni.
-mfano chambua fani na maudhui ya Kitabu cha Things fall apart kwa kingereza kisha uza kupitia mtandao wa Amazon, E bay na Lulu,
-andika Kitabu cha kufundisha lugha uijuayo mfano Kiswahili- kichina- English kisha kitafutie solo
-Anzisha Tovuti kisha andaa maudhui safi ya kufundisha lugha uijuayo kwa wageni kisha ya uze
-Andaa maudhui ya video ya kufundisha lugha kisha pakia katika mtandao wa you tube watakulipa kadiri ya wingi wa watafutaji(kumbuka kutengeneza maudhui bora na has a jifunze namna ya kutengeneza maudhui ya kufundishia kupitia google search for English..
6. Tafuta kazi za inteligensia na kijeshi katika nchi wanazohitaji. Kutokana na kukua kwa maingiliano ya watu pamoja na kuongezeka kwa ugaidi baadhi ya nchi hasa marekani na Australia wamekuwa wakiwatafuta watu wenye ujuzi wa kisomali na kiswahili na kuwaingiza katika vitengo tajwa kwaajili ya kujiimarisha kijeshi na kuimarisha usalama unaweza kuhatarishwa na wazawa wa lugha hizo. Fursa hizi tafuta katika mtandao wa indeed au google andika Swahili jobs
7. Fundisha lugha uijuayo kwa wenyeji
Shule, vyuo, na vituo mbalimbali kulingana na imahiri wako.
8. Kuwa mkalimani wa kujitegemea, kisha tafuta fursa za ukalimani wa lugha ambazo unazijua, Fanya hivi kupitia mtandao wa kazi wa indeed au tafuta kupitia google
-kila Mara jifunze namna ya kuwa mkalimani bora
-Fanya mazoezi ya kutosha ya kukalimani lugha mbili na zaidi kwa wakati mmoja
-Jifunze lugha nyingi kadiri uwezavyo kupitia mtandao.
E. Gasper
Chief in editor, masshele swahili
info.masshele@gmail.com

0 Comments