![]() |
| Picha: profesa E.Mbogo |
Muda ni asubuhi, mahali ni mlimani city, Grano coffee. Anayeanza kuingia ni E. Mashele mwandishi na mhariri mtendeji wa mtandao Huu. dakika kumi baadaye anaingia profesa Mbogo, kisha anafuatia Hagai na ndugu mwingine.
Baada ya salamu za hapa napale tunazungumza kuhusu Uandishi, mambo yanayoweza kumfanya mwandishi kuwa bora.
Kwa furaha profesa Mbogo anakiri kuwa ili mwandishi awe bora nilazima asome kazi za wasanii wengine nguli, azipitie kwa undani tena Mara kwa mara. Aidha profesa Mbogo anaongeza kuwa ili kuwa mwandishi bora wa tamthiliya nilazima mwandishi ashiriki kwa vitendo katika kuucheza mchezo huo au hata kuangalia mchezo huo ukichezwa. Hii itamwongezea mwandishi uwezo wa kuboresha matukio na namna ya kupanga wahusika pamoja na majukumu yao.
Pia kutokana na maendeleo ya kiteknolojia mwandishi anaweza kutazama michezo mbalimbali katika mtandao ya YouTube na kupata ule ufundi wa kujenga dayolojia.
Mazungumzo yananoga maswali ya hapa na pale yanachukua nafasi.
Uchapishaji binafsi(self publishing) hilo ni jambo jingine lililotawala mazungumzo. Mambo kadhaa yamezungumzwa hapa ikiwemo namna mwandishi anavyoweza kuchapa kazi zake katika mitandao ya Amazon na Lulu.com na hivyo Kitabu chake kupatikana mahali popote duniani , ukiwa ni pamoja na kuokoa gharama kubwa za uchapaji.
MKAZO
Profesa mbogo anakazia katika kufanya jambo lolote nilazima kuwe na changamoto hata hivyo nilazima mfanyaji ajitahidi kusonga mbele (ujumbe Huu ni kwa ajili ya waandishi wachanga na wote wanaoanza kufanya jambo) anaongeza mfano, ili wine ipatikane nilazima zabibu ikamuliwe, wine ni matokeo ya zabibu iliyokamuliwa.
Mwisho profesa Mbogo anapokea zawadi ya riwaya ya "Chozi la fedha haramu" iliyosainiwa na mwandishi (Emanuel Masshele) kisha kila mtu anashukuru na kuaga na kuahidi kukutana tena.
Profesa E. Mbogo ameandika vitabu lukuki vya Drama na riwaya kama vile
i.Malkia Bibi titi Mohammed
ii. Ngoma ya Ng'wana makundi
iii. Wangari Maathai
iv. Mke wangu : Alinifanya niwe mchawi
V. Fumo liongo
vi. Mondlare na samora
vii. Ujamaa utashinda?
viii. Nyerere na safari ya kanaani
ix. Niliishi dunia ya peke tangu
x. Nyota ya Tom mboya
xi. Sadaka ya john okelo
xii. Siri za maisha
xiii. Sundiata
xiv. Mtoto wa jini.
Xv. Bwana mkubwa
xvi. Giza limeingia
xvii. Tone la mwisho
xviii. Bustani ya edeni
Xix. Vipuli vya figo
Xx. Morani
Xxi. Watoto wa mama ntililie
Na kazi nyinginezo na pia anasema anaendelea kuandika

0 Comments