Picha ya njia mbalimbali katika sehemu ya Intaneti.
Intaneti (kutoka Kiingereza Internet, pia: mtandao, wavuti) ni mfumo wa kushirikiana kwa kompyuta nyingi unaowezesha tarakilishi mbalimbali duniani kuwasiliana kati yake. Kupiti le-corps.coma mtandao huo, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe.
Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mitandao ya kompyuta inayotumia itifaki inayokubalika ya intanet Suite (TCP/IP) kutumikia mabilioni ya watumiaji duniani kote. Ni mtandao wa mitandao ambayo ina mamilioni ya mitandao binafsi, mitandao ya umma, mitandao ya elimu, mitandao ya biashara, na mitandao ya serikali zenye upana wa kimitaa na kiulimwengu ambazo zimeunganishwa na safu pana ya teknolojia za mtandao za elektroniki na za mwangaza. Intaneti hubeba safu kubwa ya huduma na rasilimali za habari hasa hati za HyperText zilizoshikanishwa za Mtandao wa ulimwengu mzima (www) na miundombinu ya kusaidia barua pepe.
Mbinu nyingi za jadi za mawasiliano ya habari, kama vile huduma za simu na televisheni, zimeundwa upya kutumia teknolojia za intaneti, na kusababisha huduma kama vile itifaki ya kupitisha sauti kwa kutumia intaneti (VoIP) na IPTV. Uchapishaji magazeti umeundwa upya katika tovuti, ubadilishanaji maoni, na kupatikana habari zinapotokea tu. Intaneti imewezesha au kuharakisha uumbaji wa aina mpya za mafungamano za kibinadamu kupitia ujumbe wa moja kwa moja, majukwaa ya Intaneti na mitandao ya kijamii.
Kuna mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine na kupatikana kwa programu za kutafuta tovuti (kama google) au kwa kamusi elezo kama wikipedia.
Asili ya mtandao ina mizizi katika mwongo wa 1960 wakati Marekani ilifadhili miradi ya utafiti wa wakala zake za kijeshi na kujenga mitandao iliyosambaa ya kompyuta ambazo zina uwezo wa kustahimili mabadiliko na ni vumilivu kwa makosa. Kipindi hiki cha utafiti na ufadhili wa raia wa Marekani wa uti mpya wa mgongo uliyofanywa na msingi wa kitaifa wa sayansi ulisababisha dunia yote kushiriki katika maendeleo ya teknolojia mpya ukasababisha ufanyibiashara wa mtandao wa kimataifa katikati ya mwongo wa 1990, na kusababisha kujulikana kwa zana nyingi katika karibu kila uwanja wa maisha ya kisasa ya binadamu. Kufikia mwaka wa 2009, wastani wa robo ya idadi ya watu duniani hutumia huduma ya Intaneti.
Intaneti haina utawala wa kati katika utekelezaji wa kiteknolojia au sera ya upatikanaji na matumizi; kila mtandao jumuishi unaweka masharti yake yenyewe. Ufafanuzi tu wa majina mawili makuu katika Intaneti, itifaki ya anwani za Intanet na mfumo wa makundi ya majina, ndizo zinazongozwa na shirika iliyoagizwa ya Ushirika wa kupeana majina na nambari za intaneti (ICANN). Msingi wa kiteknolojia na masharti ya itifaki misingi (IPv4 na IPv6) ni shughuli ya kikundi maalum kilichoundwa kutekeleza kazi za uhandisi wa intaneti (IETF), ambalo ni shirika la kimataifa lisilo la kutengeneza faida ambalo washiriki wanaweza kuhusika nalo kwa kutoa mchango wa kitaalamu.
0 Comments