Header Ads Widget

Responsive Advertisement

KEN WALIBORA AMEFARIKI


Citizen TV ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyoripoti kufariki kwa mwandishi na mwanahabari ken walibora


Mwandishi nguli wa kiswahili, mwanahabari wa zamani na Mwalimu, Ken walibora  amefariki. Nguli huyo aliyejulikana kwa kalamu yake hasa katika kazi za kifasihi kama vile siku njema, Mstahiki meya, kidagaa kimemuozea, nasikia sauti ya mama, amefariki akipokea matibabu katika hospitali ya Kenyatta Nairobi. Habari zilizoufikia mtandao huu (masshele swahili) ni kuwa Ken aliripotiwa kutoweka ghafla tangu ijumaa iliyopita, Aprili 10. Ambapo kwa utafiti wa polisi pamoja na taarifa za wasamaria wema zinaonesha kuwa Walibora alihusika katika Ajali ya gari iliyotokea Landhiers Road Nairobi baada ya vitambulisho vyake kuonekana eneo hilo. Amefariki akiwa na miaka 55.

Walibora alikuwa mwajiriwa wa National media group Kenya pia amewahi kufundisha vyuo kadhaa ikiwemo chuo kikuu cha Wisconsin Marekani kama profesa msaidizi wa lugha za kiafrika vilevile katika chuo kikuu  cha Riara.

Ken lipata elimu ya juu katika shule ya Ol -kejuado high school na chuo kikuu cha Nairobi.

Atakumbukwa kwa mengi ikiwemo kazi zake mufti za kifasihi, utangazaji, tafsiri katika mtandao ya Google na Microsoft maelekezo taarifa ya English-kiswahili.

Mtandao huu unatoa pole kwa familia ya ken walibora, ndugu, jamaa na marafiki, familia ya wanakiswahili, familia ya wapenda fasihi na chama cha kiswahili duniani CHAUKIDU.

Post a Comment

0 Comments