Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MASWALI NA MAJIBU JINSI YA KUSHINDA MAMILIONI KWA WATUNZI WA USHAIRI NA NYIMBO KUPITIA TUEHU

 MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA 



1️⃣ Shindano la TUEHU ni mahususi kwa utunzi wa mashairi tu?


Ndio. Shindano la TUEHU lilianzishwa kwa lengo kuu la kuibua vipaji vya uandishi wa mashairi kwa lugha ya Kiswahili.


2️⃣ Je, mashairi yanayowasilishwa ni lazima yawe katika lughya Kiswahili?


Ndio. Ila maneno au misemo ya lugha nyingine inakubalika endapo tu ni kwaajili ya kuipa uzito wa kisanaa tungo hiyo.


3️⃣ Washairi kutoka nje ya Tanzania wanaweza kuwasilisha tungo zao kwenye shindano la TUEHU?


Hapana, shindano la TUEHU ni kwaajili ya wananchi na wakazi wa Tanzania tu.


4️⃣ Je, ni fursa gani washairi wanayopata kushiriki shindano la TUEHU?


TUEHU huibua washindi 15 kila mwaka. Tatu bora wanashinda fedha taslim: Shilingi za kitanzania milioni mbili kwa mshindi wa kwanza, shilingi milioni moja na laki saba kwa mshindi wa pili, na shilingi milioni moja na laki tatu kwa mshindi wa tatu. Washindi 12 waliosalia hukabidhiwa vyeti vya ushiriki.


5️⃣ Je, inaruhusiwa kushiriki zaidi ya mara moja?


Hapana. Mshairi hataruhusiwa kuwasilisha shairi zaidi ya mara moja kwa mwaka. Ila mshairi anaruhusiwa kushiriki shindano kila mwaka hata kama alishawahi kupata ushindi kabla.


6️⃣ Mashairi yanayowasilishwa yawe na sifa gani?


Masharti:

✅ Hili ni shindano la utunzi wa ushairi katika lugha ya Kiswahili tu.

✅ Kwa mwaka huu, tungo zitakazoshindanishwa ni za aina mbili tu: mashairi na nyimbo.

✅ Tenzi/Tendi na kazi za kinathari, kama riwaya au tamthilia, hazitahusika.

✅ Kila mshiriki awasilishe tungo moja tu.

✅ Tungo iwe ni ya mtunzi mwenyewe.

✅ Tungo iwe mpya kabisa. Yaani, isiwe imepata kuchapishwa au kutiwa katika CD au kanda; kuchezwa jukwaani, redioni au katika televisheni, au kusambazwa katika mitandao.

✅ Bahari zitakazoshindanishwa ni: Kundi A: Mashairi (ya kimapokeo au huru/masivina); Nyimbo: za kimapokeo, k.m. bongo fleva.

✅ Kila utungo wa kimapokeo uzingatie kanuni za kijadi za utunzi, na usipungue beti 7 au kuzidi beti 8.

✅ Utungo huru usipungue mishohoro (mistari) 3 wala kuzidi mishohoro 50.

✅ Kila mshiriki awasilishe tungo moja ikiwa aidha ni shairi la kimapokeo, huru-masivina au nyimbo ya bongo fleva.

✅  Mtunzi atachagua mwenyewe mada na maudhui ya utungo wake.

✅ Tungo iheshimu miiko ya kijamii na kimaadili.


7️⃣ Mashairi yanawasilishwaje?


🅰️ Mashairi yanaweza kuwasilishwa kwa kujaza fomu hii LINK: https://forms.gle/jun9yimXWrUHyshB9 


🅱️ Kwa njia ya posta kupitia sanduku la posta la shirika linalosimamia mfuko wa TUEHU, Tanzania Growth Trust (TGT). Maelezo juu ya bahasha yawe kama ifuatavyo:

Shindano la TUEHU

Tanzania Growth Trust

SLP. 8695

Dar es Salaam

Tanzania


8️⃣ Mashairi yanaruhusiwa kuwasilishwa kwa niaba ya mtunzi?


Mtunzi anaweza kupewa msaada wa kuwasilisha shairi lake lakini ni lazima shairi liwe na taarifa kamili na za kweli kuhusu mtunzi huyo. 


Kushiriki Jaza fomu hii sasa: https://forms.gle/jun9yimXWrUHyshB9 


#tuzoyaushairi #tanzania🇹🇿 #TUEHU

Post a Comment

0 Comments