Serikali nchini imeagiza uwepo wa vituo rasmi ya kujifunzia lugha ya Kiswahili katika nchi zenye balozi lengo likiwa ni kupanua matumizi ya lugha hiyo kimataifa.
Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hatua hiyo itasaidia kufungua fursa za kiuchumi ikiwemo kuwaajiri watanzania ambao watakuwa walimu wazuri kwenye ufundishaji wa lugha hiyo.
“Tunapokwenda kuwa waalimu tayari tunafungua fursa kiuchumi kuwaajiri watu, watanzani kwenda kufanya kazi na kodi itaongezeka.”amesema Majaliwa
0 Comments