Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NJIA ZITAKAZOKUEPUSHA NA MAGONJWA UKIWA CHUO

 



Habari, ndugu msomaji Leo tuangazie afya ya wanachuo. Katika makala hii utajifunza njia mbalimbali zitakazo kuweka salama ukiwa chuoni ili uweze kuendelea na masomo yako vyema.


- Epuka Ngono isiyosalama, nimuhimu kutumia Condom kwa kila tendo landoa ili kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa kama vile, kisonono, na HIV/IDS

- Jenga tabia yakucheki afya yako/zenu kabla ya kuingia katika uhusiano wa kimapenzi, hii itawaepusha Na magonjwa kama vile, Ukimwi, homa ya ini, na magojwa yanayoambukiza kwa kujamiiana.

- Epuka kushirikiana viatu, nguo nk hii itakuepusha na magonjwa ya fangasi na magonjwa mengine yangozi.


- Zingatia usafi, wa mwili, kinywa na meno, pamoja na kufanya nguo zako kuwa safi kila Mara

- Epuka kula sana Vyakula vyamafuta na vinavyotengenezwa kwa mafuta mengi.

- Fanya mazoezi kila siku, kunywa maji yakutosha pamoja nakula lishe lamili ili kuuweka mwili wako Sawa kukabiliana na magonjwa.


-  Katika kipindi hiki cha Covid-19, zingatia kanuni zote zakujikinga na magonjwa huo ukiwa nipamoja na kuvaa barakoa, kunawamikono na maji tiririka na sabuni na kuepuka kusalimiana kwa mabusu na mikono miongoni mwa kanuni nyingine.

-Epuka msongo wa mawazo hasa pale unapokosana na mwenzi wako au kufanya vibaya darasani kimasomo.



-Epuka  kuangalia mwanga wa bluu kwa muda mrefu (simu, TV, PC,)


-Pata muda wakutosha wakupumzika/kulala


Ukizingatia Haya yote Mungu atakujalia afya njema kwa muda wote uwapo chuoni 

Asante.

Post a Comment

0 Comments