Header Ads Widget

Responsive Advertisement

WANANDOA WAFARIKI BAFUNI TAHADHARI YATOLEWA



Wanandoa hao wapya Zaheer Sarang na Nabeelah Khan (24) wamefariki dunia kwa shoti ya umeme huko Afrika kusini ikiwa ni siku moja tu tangu watoke kula fungate ‘honeymoon’

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa polisi wa jimbo la Guetang, Mavela Masondo alisema miili ya wanandoa hao iligunduliwa bafuni kwao Jumapili Juni 13, mwaka huu.

 

Ilisema wanandoa hao wakiwa bafuni mke huyo alishika tap/switch akapigwa na shoti ya umeme ambapo mume alipojitosa kumuokoa na yeye akaunganishwa katika shoti hiyo wakafariki wote.

 

Aidha, taarifa za awali zinaele kuwa maeneo hayo watu hupenda kujiunganishia umeme kiholela kinyume na sheria na hivyo kusababisha majanga kama hayo.

 

Hata hivyo, polisi wamesema bado wanaendelea kuchunguza zaidi tukio hilo kwa kushirikiana na mamlaka inayohusika kusambaza umeme katika jimbo la Guetang.


TAHADHARI: usijaribu kumwokoa mtu aliyenaswa na umeme kwa kutumia sehemu ya mwili au kifaa chenye unyevu au kipitisha umeme chochote. Tumia mti mkavu  ikiwezekana zima mkondo ummeme pahala pa tukio.


Post a Comment

0 Comments