***
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kijana
mmoja mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa kata ya Ndala Manispaa ya
Shinyanga anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumuua baba yake
mzazi Shija Robert (55), kwa kumpiga na kipande cha kuni sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kumkuta amelala kitanda kimoja na mke wake.
Tukio
hilo limetokea jana usiku Aprili 26, 2022 katika mtaa wa Mwasele
Mihogoni kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo chanzo cha tukio
hilo kimetajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi baada ya marehemu kukutwa
akiwa amelala kitanda kimoja na mke wa mtuhumiwa.
Radio
Faraja imezungumza na Mwenyekiti wa mtaa wa Mwasele Mihogoni bwana
Richard Baluhi ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo ambapo
amesema mtuhumiwa huyo alienda na mke wake kumtembelea baba yake na
kwamba tukio hilo lilitokea baada ya watu hao kutumia kilevi cha pombe.
“Mimi
nilipigiwa simu nikaenda kwenye tukio nikaambia huyu marehemu ameuawa
na kijana wake mkubwa wa kwanza kumzaa, alimtembelea baba yake yeye
anaishi Ndala alikuwa na siku nne hapo kwa baba yake. Jana walitoka
kwenda kutembea walipofika wakanywa pombe wakarudi nyumbani wamelewa,
ilipofika saa nne na nusu usiku kila mmoja akaenda kulala, baada ya muda
mfupi huyu mtuhumiwa alitoka nje kwenda chooni kujisaidia haja ndogo”,amesema.
“Aliporudi
huyo baba mtu alishanigia kwa mke wake na huyo mtuhumiwa na kwa sababu
hiyo nyumba haina taa basi huyo kijana alikuwa na tochi alipomulika
akamuona baba yake amelala kitanda kimoja na mke wake basi wakaanza
kupigana humo ndani na baadae wakatoana nje, huyo kijana alichukua
kipande cha kuni ndipo akaanza mashambulizi akampiga mpaka kufa”, ameeleza mwenyekiti Baluhi
Kamanda
wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Polisi George Kyando
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema tayari jeshi la
polisi linamshikilia mtuhumiwa huyo huku likiendela kufanya uchunguzi
zaidi.
Chanzo - Radio Faraja
0 Comments