JAMES Kwasi raia wa Ghana na nyota wa zamani wa Asante Kotoko
anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Simba kurithi mikoba ya Pablo
Franco.
Kwasi yeye zama za uchezaji wake alikuwa anacheza nafasi ya ulinzi ambapo alikuwa ni beki wa kushoto.
Taarifa zinaeleza kwamba Simba wapo kwenye mazungumzo na kocha huyo raia wa Ghana ili aweze kuwa nao kwa msimu wa 2021/22.
Rekodi zake zinaonyeshwa kwamba mwamba huyo aliletwa duniani Agosti 9
1959 amecheza kwa mafanikio kwenye timu ya Taifa ya Ghana na ile Kumasi
Asante Kotoko ambapo aliweza kuzifundisha zote kwa nyakati tofauti.
Aliweza kuwa nahodha kwenye timu ya Taifa ya Ghana na Asante Kotoko 1988-92.
Aliwahi kuifundisha Asante Kotoko akiwa ni kocha msaidizi 1993-95 na alikuwa kocha mkuu kwenye timu hiyo 1995-96.
2000-01 alikuwa ni kocha msaidizi kwenye timu ya Taifa ya
Ghana,maarufu kama Black Stars ambayo hata 2008 aliwahi kuifundisha pia
hata 2017/19
2012 alikuwa ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Ghana kwa vijana chini ya miaka 23.
2014-15 alikuwa ni Kocha Mkuu wa Al Khortoum FC ya Sudan.
Kocha huyo ni miongoni mwa makocha ambao wana leseni A ya Caf hivyo
akitua ni uhakika kukaa kwenye benchi kwenye mechi za kimataifa ambapo
Simba inatarajiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika rekodi za mafanikio aliwahi kutwaamataji matatu akiwa na timu
ya Asante Kotoko ilikuwa ni 1995/96 ambapo pia alishinda medali ya
Silva.
2009 katika mashindano ya Afcon aliweza kupewa tuzo ya medali ya Silva kwenye Afcon.
2012 aliweza kutinga hatua ya nusu fainali ya Afcon iliyofanyika
Equatorial Guinea na 2013 aliweza kuongoza timu ya taifa ya Ghana
kutinga hatua ya nusu fainali ya Afcon na 2019.
0 Comments