Malkia Elizabeth II wa Uingereza, malkia aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi duniani, afariki dunia akiwa na umri wa miaka 96.
Malkia Elizabeth wa pili amefariki Leo Sept.8,2022.
Malkia Elizabeth wa pili,alirithi madaraka kutoka kwa Baba yake ,Mfalme George wa sita 1952. Mfalme George wa sita hakuwa na Mtoto wa kiume ,kama laiti angelikuwa na Mtoto wa kiume basi mtoto huyo wa kiume angerithi kiti cha ufalme.
Bahati mbaya Mfalme George aliyetawala kuanzia Desemba 11 ,1936 hadi Februari 6 ,1952 alizaa watoto wawili tuu wote wa kike ,mmoja ni Elizabeth ambaye ndiyo wa kwanza na wapili ni Margaret.
Mfalme George alipofariki 1952 ,Mtoto wake wa Kwanza Elizabeth akaridhi mamlaka hivyo kuitwa Malkia Elizabeth II wa pili tangu 1952 hadi 2022 , vyema kujua huyu ni Malkia Elizabeth wa pili ni tofauti na Malkia Elizabeth I wa Kwanza .
Malkia Elizabeth I wa kwanza alikuwa Malkia wa Uingereza na Ireland kutoka 1558 hadi 1603, mwisho wa watawala wa Tudor .
Huyu aliyefariki ni Malkia Elizabeth wa pili alitawala kutoka 1952 hadi kifo chake leo Sept.8 ,2022 ,ndiyo maana tangu tunazaliwa hadi sasa tulikuwa tunasikia tuu Malkia Elizabeth ,Malkia Elizabeth.
Malkia Elizabeth aliolewa na Prince Philip ,sheria inakataza mume kuwa na nafasi ya ufalme sababu nafasi yao ni ya kurithi ndani ya udugu wa damu tangu miaka na miaka.
Kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth ,mtoto wake mkubwa Charles ndiye sasa amechukua nafasi na kiti hivyo anaitwa Mfalme Charles wa Uingereza (King Charles).
Mfalme Charles ana miaka 73 ,ndiye mtoto mkubwa wa Malkia Elizabeth kati ya watoto wake 4 ,aliyezaa na hayati mume wake Prince Philip ambaye alifariki mwaka uliopita.
Hivyo jina Sasa sio tena Malkia ,kama tulivyozoea sasa ni Mfalme Charles wa uingereza.
Mungu amlaze panapostahili Malkia Elizabeth.

0 Comments