
Chanzo cha picha, Reuters
Joao Felix
Arsenal imepewa nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 23, kutoka Atletico Madrid mwezi Januari, mbele ya Paris St-Germain, Manchester United na Aston Villa. (Marca AS in Spanish)
Kuna "nafasi nzuri" Arsenal wataweza kumsajili winga wa Ukraine Mykhaylo Mudryk mwezi Januari, kwa chini ya dau la £86m ambalo Shakhtar Donetsk ilikuwa ikitaka kutoka kwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Athletic)
Liverpool wana makubaliano kimsingi na Benfica kumsaini kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, 21. (La Capital - kwa Kihispania)
Fernandez ni mbadala wa Real Madrid ikiwa hawataweza kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund kwa msimu ujao. (Sport – AS In Spanish)

Chanzo cha picha, BBC and Twitter
Enzo fernanndez
Shirika la Soka England linamtaka Gareth Southgate kuendelea kuwa meneja wa England, licha ya kupima nia ya kocha wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel katika kazi hiyo kabla ya Kombe la Dunia. (Bild - in Germany )
FA itazingatia kocha wa kigeni ikiwa Southgate atajiuzulu kama meneja wa Uingereza. (Telegraph -Subscription required )
FA inamwona kocha wa Leicester City, Ireland Kaskazini, Brendan Rodgers kama kocha mwenye nafasi nzuri - lakini sio Frank Lampard au Steven Gerrard. (Star)
Brazil wanamtaka Carlo Ancelotti kurithi mikoba ya Tite kama kocha baada ya kutumwa kwenye Kombe la Dunia, na kuwasiliana na Real Madrid kwa njia isiyo rasmi mwezi Oktoba. (UOL Esporte – In Portuguese)

Kiungo wa Leicester City Youri Tielemans
Leicester City wanajiandaa na Arsenal kufanya jaribio la mwisho la kumnunua Youri Tielemans mwezi ujao kabla ya kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji, 25, kuwa mchezaji msimu msimu wa joto. (Mirror)
Chelsea wameanza mazungumzo ya kumsajili mchezaji wa Ujerumani Youssoufa Moukoko, 18, kwa uhamisho wa bila malipo kutoka Borussia Dortmund mwezi Julai. (Nicolo Schira)
Paris St-Germain wana nia ya kumsajili winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 25, kutoka Barcelona. (El Nacional - kwa Kikatalani)
AC Milan wako kwenye mazungumzo na mchezaji anayesakwa na Chelsea na Manchester United Rafael Leao kuhusu kuongezwa kwa mkataba, na wamenyamaza " kuhusu iwapo mshambuliaji huyo wa Ureno, 23, atasaini mkataba mpya. (Gazzetta dello Sport, Through Goal )
Manchester United itaweka wazi kifungu cha kuongeza kandarasi kwa mlinda mlango wa zamani wa Uhispania David de Gea, 32, beki wa kushoto wa Uingereza Luke Shaw, 27, na kiungo wa kati wa Brazil Fred, 29, pamoja na mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 25, na mlinzi wa kulia wa Ureno Diogo Dalot, 23. (Manchester Evening News)
Leeds United wanapanga kumnunua beki wa kushoto wa PSV Eindhoven wa Ujerumani Philipp Max, 29 Januari. (Football Insider)
Wilfried Zaha, 30, anaonekana kuwa na uwezekano wa kuondoka Crystal Palace kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ivory Coast utakapokamilika msimu ujao. (Fabrizio Romano, through CaughtOffside)
Sevilla wanataka Isco aondoke Januari, miezi mitano tu baada ya kumsajili kiungo huyo wa zamani wa Uhispania, 30, kutoka Real Madrid. (Marca in Spanish)
Bayern Munich wanakaribia kuafikia makubaliano ya kumnunua kiungo wa kati wa Austria Konrad Laimer, 25, kwa uhamisho wa bure kutoka RB Leipzig msimu ujao wa joto. (Fabrizio Romano)
Tottenham Hotspur iko tayari kufanya mazungumzo mapya na meneja Antonio Conte wiki hii kuhusu kandarasi mpya ya muda mrefu kwa Muitaliano huyo. (Athletic)
Kocha wa zamani wa Barcelona na Roma Luis Enrique anataka kurejea katika kazi ya klabu baada ya kuacha nafasi yake ya ukocha wa Uhispania. (Sport – In Spanish)
Meneja wa zamani wa Tottenham na Paris St-Germain Mauricio Pochettino amewaambia marafiki zake kwamba anatamani sana kibarua cha Chelsea, iwapo kitapatikana. (Football Insider)
Amazon ndio kampuni ya hivi punde zaidi kuhusishwa na kununua Manchester United - lakini bei ya familia ya Glazers ya takriban £7bn inaaminika kuwa isiyowezekana na wataalam wa sekta hiyo. (Mail)
0 Comments