Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SADAKA YA JOHN OKELLO

 

TAMTHILIYA ya SADAKA ya John okello
SADAKA YA JOHN OKELLO TAMTHILIYA

Sadaka ya John Okello ni tamthilia ya kihistoria kuhusu mapinduzi ya tarehe 1/12/1964 visiwani Zanzibar. Wakoloni Waingereza, kabla ya kuondoka visiwani walimkabidhi Sultani Jamshid uhuru na mamlaka ya kuitawala Zanzibar tarehe 01/12/1963. Wazanzibar wengi na hasa Waafrika weusi, waliona kuwa ule ulikuwa uhuru bandia uliokuwa na lengo la kuendeleza usultani, umwinyi na ukandamizwaji. Katikati ya fukuto na taharuki hii, chama cha Afro-Shiraz Party- cha Amani Abed Karume na Umma Party cha Abdulrahaman Babu, miongoni mwa vyama vingine, viliwahamasisha vijana kushika silaha dhihi ya Usultani. Mtu mmoja, Field Marshall John Okello, kijana mwenye asili ya Uganda, ambaye vitabu vya Historia vimemsahau, alikuwa mstari wa mbele katika kupanga na kutekeleza mapinduzi haya yaliyomng'oa Sultan Jamshid usiku wa kuamkia tarehe 12 Januari 1964.

Chapisho la mdau Jamiiforums

Mwaka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?


1332A8BF-A6E5-4160-B936-43321E10066E.jpeg



Post a Comment

0 Comments