Takadini alikuwa sope yaani zeruzeru na hatimaye alipata ulemavu, akatengwa na watoto wenzake huku wengine wakimkejeli. katikati ya unyonge na mashaka, Takadini na mama yake wanafarijika kwa mapenzi wanayopewa na Baba Chivero, mganga mshauri ambaye kabla hajafa anamfundisha Takadini tiba mbalimbali. Hata Takadini anapoibuka kuwa mpigaji mbira hodari, hatimaye jamii inaanza kuvutiwa naye. Akatokea msichana akampenda, wakaoana na wakapata mtoto asiye sope. Kumbe ulemavu wake na uzeruzeru wake, havikumzuia kuyatenda yale wafanyayo binaadamu wengine. Je, taswira hiyo ya mila dhidi ya masope ingepokewaje na jamii ya mama yake Takadinii pindi watakaporeje?

0 Comments