SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na.JA.9/259/01/A/326
30/06/2023
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara za
Serikali, Wakala wa Serikali, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (MDA’s- & LGA’s)
anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kwa nafasi ya Afisa Maendeleo
ya Jamii II kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 08-07-2023 hadi 18-07-2023
na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa
wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na
sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kituo cha Usaili.
ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha
Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Leseni ya Udereva, Hati ya
kusafiria au barua kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unakatoka.
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,
kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana
na sifa za Mwombaji.
vi. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results,
hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA
NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
ix. Kwa wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na
kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xi. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na
kunakili namba ya usaili kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
x. Vifaa vya kieletronic haviruhusiwi
Kupakua Majina Bofya >>HAPA>>
.jpeg)
0 Comments