Header Ads Widget

Responsive Advertisement

ARSENAL WENGER OZILI NA SANCHEZ HAWAUZWI

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema Mesut Ozil na Alexis Sanchez hawauzwi, hata kama hawatakubali kuongeza mkataba.

Nyota hao wa Gunners kwa pamoja wamefunga mabao 21, huku wakiwa wamebakiza miezi 18 kwenye mikataba yao na Wenger ana matumaini ya kuwabakiza hadi baada ya mikataba yao kumalizika mwaka 2018.

Wakati kocha huyo wa Arsenal akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchezo wao wa kesho dhidi ya Stoke City, aliwatuliza mashabiki wa klabu hiyo kwamba hawana mpango wa kuwapoteza wachezaji hao.

“Hata iweje watabaki kumaliza miezi yao 18 na zaidi,” alisema Wenger.

Wenger hajakanusha kutakiwa kwa Sanchez na klabu za China, lakini alisema: “Kwanini uende China wakati huu ambao bado unacheza England?”

“Ila mara zote mmekuwa mkiuliza kitu kimoja, ila hilo haliongezi kasi ya makubaliano ya mkataba.

“Mnapaswa kuheshimu utaratibu, kuna wakati unakuwa na kasi, mara nyingine taratibu na mkiona makubaliano yanachelewa mnauliza katika kila mkutano wa waandishi.”

Alipoulizwa kama mazungumzo hayo yanayoendelea yanaweza kuiathiri Arsenal kwenye chumba cha kubadilishia na kusema kwamba, Ozil na Sanchez wanatimiza majukumu yao.

“Hii ni kazi yetu, miezi 18 ni muda mrefu sana na siamini kwamba hilo ni tatizo.”


London uingereza


Post a Comment

0 Comments