Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MAAJABU YA LUGHA YA KISWAHILI

        Toggle navigation Menu 04:25Bahati MtilaNo comments MAAJABU YA LUGHA YA KISWAHILI. MAAJABU YA LUGHA YA KISWAHILI Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kibantu yenye asili ya mwambao wa pwani ya afrika mashariki yenye lahaja mbalimbali na ambayo hutumiwa na watu wengi wa afrika mashariki na kati mfano Kenya ,Rwanda,Burundi,Congo na hususani Tanzania. Maajabu ni mambo ya kushangaza ,yasiyokuwa ya kawaida na yenye upekee mkubwa ukilinganisha na hali ya kawaida. Maajabu ya lugha ya Kiswahili ni upekee , hali isiyokuwa ya kawaida ,ubunifu na umahili ndani ya lugha ya Kiswahili jinsi inavyopendeza ,inavyovutia na inavyotumika ndani ya jamii mbalimbali .Kuna maajabu mbalimbali ndani ya lugha ya Kiswahili lakini yafuatayo ni maajabu saba ya lugha ya Kiswahili :- Asili ya lugha ya Kiswahili; lugha ya Kiswahili asili yake ni mwambao wa pwani ya afrika mashariki ambao huhusisha nchi kama Kenya na Tanzania .Asili hii ya lugha ya Kiswahili tunaweza kusibitisha kwa sababu mbalimbali kwa mfano lahaja nyingi za Kiswahili zinapatikana ndani ya afrika mashariki, waongeaji wazuri wa lugha ya Kiswahili wanapatikana ndani ya afrika mashariki na waandishi wengi wa vitabu vya Kiswahili bado wanapatikana ndani ya afrika mashariki. Hivyo basi hii inathibitisha kuwa Kiswahili kina maajabu makubwa. Fasihi ya lugha ya lugha ya Kiswahili, fasihi ya lugha hii ni ya pekee sana ukilinganisha lugha zingine mfano katika tanzu kama vile Liwaya ,Tamthilia na Ushairi, kwa kiasi kikubwa tanzu hizi zinaingiliana na kutofautana mfana tamthilia ya Nguzo Mama ya Penina Muhando tunaona anajaribu kutumia nyimbo katika kuisana kazi yake ambao ni kipera cha ushairi. Hivyo basi haya ni maajabu ndani ya lugha Kiswahili katika fasihi ya Kiswahili. Ukuaji na ueneaji wa lugha ya Kiswahili, hapa tunaangalia njia mbalimbali zinazotumika kukuza na kueneza lugha hii ya Kiswahili mfano vyombo vya habari kama vile Lungoya (redio japan idhaa ya Kiswahili) ,sauti ya amerika kwa lugha ya Kiswahili hii ni kwa upande wa nje ya afrika mashariki.pia kuna taasisi pamoja na vyama mbalimbali vinavyoshughulikia na ukuzaji na uenezaji wa lugha hii ndani ya afrika mashariki mfano TUKI ,TAKILUKI ,CHAWAKAMA,BAKITA,UKUTA nakadhalika. Hivyo basi hii inapelekea idadi ya watumiaji kuongezeka na kukifanya Kiswahili kuendelea kuwa na maajabu makubwa. Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika muktadha mbalimbali, mfano elimu,siasa, uchumi, michezo,mikutano ,sherehe na mahubiri.kwa kuanza na muktadha wa elimu Kiswahili kimepandishwa hadhi mpaka kufundishwa ngazi ya chuo kikuu, sekondari kama somo na shule za msingi kama lugha ya kufundishia masomo yote isipokuwa kiingereza tu ndani ya Tanzania pia Kiswahili kutumika kwenye mikutano mikubwa ndani ya afrika mfano ya jumuiya wanachama wa afrika mashariki. hivyo basi hayo ni maajabu makubwa ndani ya lugha hii. Uundaji wa msamiati wa lugha ya Kiswahili. msamiati ni maneno yanayopatikana katika lugha Fulani hivyo basi msamiati katika lugha ya Kiswahili ni maneno yanayopatikana ndani ya lugha ya Kiswahili. Lugha hii ina njia nyingi sana zinazotumika katika kukuza msamiati wake kama vile kutohoa toka lugha za kigeni, miambatano, kufananisha umbo sura na sauti, na kubadilisha mpangilio wa herufi.hizi njia zinazotumika katika kuundia msamiati wa lugha ya Kiswahili. Utafutaji na upataji wa visawe vipya vya lugha ya kiswahli. Visawe ni maneno ndani ya lugha mbalimbali yanayofafanua kitu au jambo moja kwa matamshi ya lugha hizo. Katika lugha ya Kiswahili kuna uhaba wa visawe vinavyotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia lakini jitihada zimefanyika na zinaendelea kufanyika katika kuhakikisha visawe vinapatikana mfano wa visawe vipya ni mnyange, nywila, kinuruweo, sasisha, talakilishi, talakilishi mpakato pamoja na kinyoni. Hivyo basi haya ni maajabu makubwa sana yanayopatikana ndani ya lugha hii ya Kiswahili. Kasumba na uhaba wa wataalamu wa lugha ya Kiswahili. Kasumba ni hali ya kutothamini kitu chako kwa kung’ang’ania vitu vya kigeni.hili ni moja ya ajabu katika lugha ya Kiswahili kwa sababu wazawa wengi hususani wasomi wanakidharau kiswahli japo kuwa ndio lugha yao pia licha ya kuwa Kiswahili asili yake ni afrika mashariki ajabu bado kuna uhaba wa wataalamu wa lugha hii. Hivyo basi hayo yote yanabaki kama maajabu katika mlongo hasi. Hivyo basi hayo ndio maaajabu ya lugha ya Kiswahili. Ili kiswahili kiweze kuendelea zaidi na zaidi ni lazima elimu itolewe juu ya umuhimu wa lugha hii.pia serikali ni lazima itambue kuwa hii ni lasilimali hivyo basi ni lazima iwekeze vya kutosha kwa kushilikiana na vyombo vyombo vya habari, wadau mbalimbali, mashirika mbalimbali , pamoja na taasisi na vyama mbalimbali vya kukuza na kuendelza Kiswahili ndani na nje ya nchi. 

Post a Comment

0 Comments