Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Sauti za kiswahili , Sauti ghuna na siighuna

Sauti za Kiswahili SAUTI ZA KISWAHILI KitengoMuundo wa Neno Aina Kuu Konsonanti Irabu NAVIGATION NextMofimu PrevShadda na Kiimbo a, b, ch, d, e, f, g, h, i, k, l, m, n, o, p, r, s, t, u, v, w, y, z Kuna aina mbili za Sauti katika lugha ya Kiswahili: Irabu Konsonanti Irabu (Vokali) a, e, i, o, u Irabu zinapotamkwa, hewa haizuiliwi katika ala za matamshi. Jedwali lifuatalo litakuonyesha jinsi ya kubainisha vokali kulingana na sehemu ya ulimi inayoachilia hewa, na jinsi midomo inavyobadilika IrabuSehemu ya UlimiMidomo e,iMbeleMidomo imetandazwa aKatikati; ulimi huinuka na kutandazaMidomo imetandazwa o,uNyumaMidomo imevirigwa Konsonanti b, ch, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, r, s, t, v,w, y, z Konsontanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa katika ala za matamshi ( ulimi na midomo). Kuna aina mbili kuu za sauti za konsonanti: Sauti Ghuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa hutikisa nyuzi za sauti Sauti Sighuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa haitikisi nyuzi za sauti Jedwali lifuatalo litakuonyesha aina za konsonanti kulingana na mahali zinapotamkiwa na sauti (ghuna au sighuna) MidomoMidomo + MenoMeno + UlimiUfiziKaakaa + ufiziKaakaa gumuKaakaa LainiKooAina ya Sauti Vipasuop dt djk gsighuna ghuna Vikwamizo / Vikwaruzof vth dhs zshkh ghhsighuna ghuna Kipasuo - kwamizochsighuna Nazali / Ving'ong'omnnyng'ghuna Kitambazalghuna Kimadenderghuna Viyeyusho / Nusu Irabuywghuna Vipasuo ( p,b,k,g,t,d ) Hutamkwa kwa kukutanisha ala za kutamkia ili kufungilia hewa na kisha kuiachilia ghafla Vipasuo sighuna (p, k, t ) - hutamkwa bila kutikisa nyuzi za sauti Vipasuo ghuna (b, g, d ) - hutamkwa kwa kutikisa nyuzi za sauti /p/ na /b/ hutamkwa kwa kukutanisha midomo katika meno: /p/ - papa, pepea, pipi, popo, pua /b/ - baba, bebea, bibi, bobo, bubu /t/ na /d/ hutamkwa kwa kukutanisha ufizi na ncha ya ulimi /t/ - taa, tetea, titi, toto, tua /d/ dada, doa, dua /k/ na /g/ hutamkwa kwa kukutanisha nyuma ya ulimi na kaakaa laini /k/ - kaka, koko, kuku /g/ - gae, gege, gogo, gugu Vikwamizo ( d f,v,dh,th, s,z,sh,h,gh) Pia huitwa Vikwaruzo Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kisha kuachilia hewa kupitia katika mwanya mwembamba Vikwamizo sighuna (f,th,s,kh,h,sh) - hewa haitikisi nyuzi za sauti Vikwamizo ghuna (v, dh,z,gh) - hewa hutikisa nyuzi za sauti /f/ na /v/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa chini na wa juu na kuachilia hewa kidogo kupita /f/ - faa, fee, fua /v/ - vaa, vua /s/ na /z/ hutamkwa kwa kukutanisha sehemu ya kati ya ulimi na kaakaa gumu /s/ - sasa, sisi /z/ - zaa, zeze, zizi, zuzu /dh/ na /th/ hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na meno ya juu /dh/ - dharau, dhani /th/ - thubutu /gh/ na /kh/ hutamkwa kwa kukutanisha kaakaa laini na kilimi /dh/ - dharau, dhani /th/ - thubutu /h/ hutamkwa kwa kukutanisha kilimi na koo na kuachilia hewa kwa nguvu /h/ - haha, hii, huu Kipasuo-kwamizo: ( ch ) Pia huitwa kituo-kwamizo - Hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, na kuachilia hewa /ch/ - chacha, chechea, choo Ving'ong'o / Nazali ( m,n,ng',ny ) Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kuzuia hewa kupitia kinywani; hewa hupitia puani. /m/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa juu na wa chini, ili kuzuia pumzi kupita kinywani /m/ - mama, umeme, mimi, /n/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, ili hewa ipitie puani /n/ - nana, nene, nini, nono, nunua /ny/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa gumu /ny/ - nyanya, nyenyea, nyinyi, nyoa, nyunyu /ng'/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa laini /ng'/ - ng'ang'a, ng'oa Kitambaza ( l ) Hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi huku hewa ikipitia kwenye pande za ulimi bila kukwaruza ufizi /l/ - lala, lea, lilia, lo! lulu Kimadende ( r ) Hutamkwa kwa kupigapiga na kukwaruza ufizi haraka haraka kwa ncha ya ulimi. /r/ - rai, rarua, Viyeyusho ( y,w ) Pia huitwa nusu-irabu. Hutamkwa kwa utaratibu kwa kuleta ala za matamshi karibu sana lakini kuachilia hewa bila kuikwaruza. /w/ hutamkwa midomo ikiwa wazi /w/ - wawa, wewe, /y/ hutamkiwa kwenye kaakaa gumu /y/ - yaya, yeye, Ala za Kutamkia Hizi ni sehemu za mwili zinazotumika wakati wa kutamkia maneno: Meno, Ulimi, Midomo, Pua, Chemba cha Pua, Ufizi, Kaakaa gumu, Kaakaa laini, Kimio , Chemba cha Kinywa, Ncha ya ulimi, Bapa la ulimi, Shina la Ulimi, Koromeo, Kidakatonge, Kongomeo, Nyuzi za Sauti, Koo, Njia s

Post a Comment

0 Comments