MKASA WA KUSISIMUA JUMATATU
HII YA PASAKA: "HAKUFA VITANI, AMEKUFA NYUMBANI"
#inasikitisha sana
kutokana na kazi yake ya uanajeshi ilimlazimu kuwa mbali na familia kwa mda, alimuacha mkewe na mwanae wa kike mwenye miaka miwili akaenda kupigania nchi yake ya India kule Pakistan, alikaa vitani miaka kadhaa, vita ilipoisha walirudishwa India serikali ikawazawadia wanajeshi wote waliokua vitani kila mmoja gari jipya la kifahari na kitita cha fedha kama pongezi kwao kwa kulipigania taifa, alirudi nyumbani, alifurahi mno kumkuta mtoto wake kakua sasa ni binti wa darasa la kwanza anajua hadi kusoma na kuandika
Furaha ilikua kubwa mno katika familia, binti yule ambaye ndie mwanae wa pekee alikua faraja kubwa mno kwake baada ya stress za vita, alijivunia sana uwepo wa mwanae,
Hakika alizidi kumpenda sana mkewe na mtoto wake, muda mwingi alipenda kukaa karibu na mwanae akimhadithia simulizi nzuri za kusisimua za kale. Ila vita ilikua imeshamuathiri, kichwa chake maskini hakikua sawa tena kama zamani, uwezo wake wa kujicontrol na kudhibiti hisia kali ikiwemo hasira hakuwa nao tena,
Siku moja Wakati baba akiwa anasafisha gari yake , mwanae alichukua jiwe na kuanza kuandika katika upande wa lile gari.
Kwa hasira baba alichukua mkono wa yule mtoto na kuanza kumpiga kwa nguvu bila kugundua kuwa alikua akitumia spana kumpigia hivyo akamuumiza vibaya.
Hospitalini wakapata report kuwa mtoto ameumia vibaya kupelekea mifupa ya vidole vyote kuvunjika hivyo inatakiwa kuondoa vidole vyote.
Mtoto alipomuona baba yake kwa uchungu na maumivu makali akamuuliza "Baba ni lini vidole vyangu vitarudi tena?" Baba aliumia vibaya sana moyoni na hakika hakua na la kusema.
Alirudi nyumbani na kulipiga gari lake mara nyingi kwa hasira, akiwa amekaa upande wa lile gari akatazama ni nini mwanae alichokua akiandika. Kuja kuona mwanae aliandika "NAKUPENDA SANA BABA YANGU". Siku iliyofuata Baba alijinyonga baada ya kushindwa kuhimili hisia za alichokifanya kwa mwanae.
FUNZO KUU
Stress za kimaisha na kimaendeleo unazopitia kila siku ndio vita yako sasa ndugu yangu unaesoma mkasa huu, epuka changamoto za kimaisha kupoteza uwezo wako wa kudhibiti akili yako na kushindwa kufanya maamuzi sahihi katika ndoa, familia, uhusiano na maisha yako kwa ujumla, hasara ya kukosa SELF CONTROL ni kubwa, waeza jikuta kutokana na stress umempiga mkeo vibaya, umemtukana mzazi, umegombana na ndugu au hata kujeruhi au kusababisha mauaji. JIFUNZE KUJIDHIBITI MAANA MAJUTO NI MJUKUU.
Madhara mengine ya mtu kuruhusu stress kumtawala tumeona tena hapo baada ya kugundua makosa yake ameamua kujinyonga hakika hakukuwa na haja ya kujiua bali ilikua ni suala la kufikiria namna ya kumsaidia mwanae siku za badae, huenda kuachwa kwako, kusalitiwa, kufukuzwa kazi n.k kumekuchanganya hadi wafikiria kujiua ila tambua BADO UNATEGEMEWA MNO na mchango wako ni wa muhimu mno.
MAPENZI NA HASIRA.
Hivi vitu viwili havina mipaka, chagua upendo ili uweze kuishi vizuri hapa duniani na achana na hasira. Vitu vinatakiwa kutumiwa na watu wanatakiwa kupendwa.
Ila kwa bahati mbaya dunia ya sasahivi mambo yamebadilika sana vitu vinapendwa na watu wanatumiwa.
Angalia mawazo yako huja kuwa maneno, angalia maneno yako huja kuwa matendo, angalia matendo yako huja kuwa tabia, angalia tabia yako huja kuwa mazoea na angalia mazoea yako huja kuwa ndio mwisho wako.
Unajua uhusiano uliopo kati ya macho yako? Yanalia pamoja, yanafumba pamoja na panapo furaha hufurahi pamoja ingawa hayajawahi kuonana hata siku moja. Marafiki ni nguzo mojawapo ya maisha na upendo ndio msingi wa maisha.
Let love lead.
🌹🍎❤❤❤❤❤❤❤🍎🌹
Nakutakia Jumapili Njema ya PASAKA usherehekee kwa amani na furaha, pia nicheki whatsapp 0766605392

0 Comments