Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kimenukaa: Jeshi la Polisi Latangaza Vita ..Lajiandaa Kuvamia Mkoa wa Pwani kijeshi Kupambana na Majambazi Walioua Askari.!!

Kimenukaa: Jeshi la Polisi Latangaza Vita ..Lajiandaa Kuvamia Mkoa wa Pwani kijeshi Kupambana na Majambazi Walioua Askari.!!

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani ameongea na waandishi wa habari mchana huu na kutolea ufafanuzi tukio la mauaji ya Askari Polisi 8 lililotokea jana jioni huko Kibiti, Pwani.
CP Marijani ameeleza kuwa tukio hilo sio la kigaidi kama ambavyo imekuwa ikivumishwa, bali ni tukio la kawaida la ujambazi ambalo halililazimu Jeshi la Polisi kuunda Kanda Maalumu ya Kipolisi kwa Mkoa wa Pwani.
Aidha, amesisitiza kuwa, hilo ni tukio la kawaida na wala sio tukio la kutisha na kuzua hofu bali imetokea tu bahati mbaya mapolisi kuuawa na wao kama Jeshi Imara watazidisha mapambano na kudumisha ulinzi.
Mpaka sasa, wameshajibu mashambulizi yaliyowalaza chini majambazi 4 na idadi yao itaongeza kwa kuwa imeundwa operesheni maalumu ambayo haitokuwa na mzaha wala msamaha.

Post a Comment

0 Comments