Kukosea kumefanya watu kujidharau na kurudi nyuma katika hatua zao. Naamini utakubaliana nami kuwa ni Mara nyingi tumekuwa tukijuta na kuumia na wengine hata kulia tukikumbuka Yale tuliyoyafanya nyuma. Lakini umeshawahi kujiuliza baada ya uchungu huo na maumivu ni nini kitafata!??
Je utaendelea kulia kila siku na kuumia na kuishi maisha ya kujilaumu kwa makosa yako??!!
Je kitabadilika nini baada ya majuto hayo ??
Jibu la haraka ni kuwa hakuna kitakachobadilika na hapa ndio nakumbuka ule msemo wa Yaliyopita si ndwele tugange yajayo
Ni lazima Leo uamue kuishi maisha mapya ,kukubali kuwa MTU mpya, kufanya mambo mapya na kuchukua hatua nyingine
Usikubali kurudi nyuma, USIJILAUMU, USILIE, USIJUTE kwa yaliyotokea usikubali maisha yako ya sasa yalinganishwe na Yale ya Jana.
JISAMEHE, SIMAMA, ANZA hatua mpya Leo.
Kubali kujifunza kwa Yale uliyokosea lakini kamwe usikubali makosa yako yaharibu maisha yako ya sasa au yakufanye uonekane MTU mbaya.
Kumbuka KUTELEZA si KUANGUKA. Kila siku ujiambie LEO NIMEKUWA BORA ZAIDI YA JANA na Kuanguka kumenifundisha kusimama.
2 Comments
Jisamehe, Simama anza Upya leo. Hakika kweli leo nimejifunza kitu kikubwa sana maishani mwangu.
ReplyDeleteAsante.
ReplyDelete