Header Ads Widget

Responsive Advertisement

LUCKY NUMBER: NAMBA YAKO YABAHATI NAMICHEZO UNAYOWEZA KUSHINDA

@From: maalim hassan 
Kila mtu anataka kujua namba yake ya bahati na namna ya kuitumia kwa faida yake. Baadhi ya watu wanataka kutumia namba zao za bahati kwa kupanga tarehe zao muhimu na kufanya maamuzi au kwa kufanya usaili (Interviews). Wengine wanataka kujua namba zao za bahati kwa ajili ya starehe zao, kufunga ndoa au kwa mafanikio ya mipango yao.
Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni ipi namba yako ya bahati, cha pili ni jinsi gani ya kuongeza nguvu ya bahati ya namba yako ya bahati pindi unapoijua. Namba yako muhimu au ya bahati inatokana na tarehe yako ya kuzaliwa .
Miaka elfu iliyopita ya uchunguzi ya wale waliokua na hamu ya kujua siri na nguvu za nambari wamethibitisha kwamba tarehe yako ya kuzaliwa ni namba yako ya bahati na namba muhimu sana kwako. Kwa mfano tuchukulie mtu alizaliwa tarehe 14 th Agosti (1+4=5) namba (5) ndio namba yako ya bahati na mtu aliyezaliwa tarehe 7 th Dec namba (7 ) ndio namba yake ya bahati.
Sasa basi umejua namba yako ya bahati je ni vipi utaiongezea nguvu ya bahati. Kwanza ni lazima uanze kuitafakari namba hiyo (Concentrate on that namber). Anza kuitazamia namba hiyo siku itakayo jitokeza kwenye kalenda kila mwezi. Mfano ikiwa namba yako ya bahati ni 5 basi kila tarehe itakayo jumlishakupat tano ndio siku yako ya bahati mfano tarehe: 5 14 23 (5) 14 (1+4=5) 23 (2+3=5) hizi ni tarehe zinzoweza kukupa nafasi kubwa ya mafanikio. Na mtu aliyezaliwa tarehe 3 basi ni sawa na mtu aliyezaliwa tarehe 12(1+2=3), 21(2+1=3) na 30(3+0=3) na yao bahati ni 3. Sheria hii inatumika kwa number zote ispokua na 4 na 8 kutokana na mabadiliko yake ya ghafla na matatizo nguvu zake hazitakiwi kuongezwa
Watu waliozaliwa tarehe 4 na 8 namba hizi hukumbana na matatizo na mikosi mara kwa mara kuliko namba zingine zozote kwa hiyo wanashauriwa mwenye namba 4 atumie namba 1 ambayo ni sawa na 10(1+0=1) 19 (1+9=10 1+0=1) na 28 92+8=10 1+0=1) na mtu wa namba 8 atumie namba 3 ambayo ni sawa na 12(1+2=3) 21(2+1=3) na 30(3+0=3) kwa kufanya mipango na mikakati yake muhimu.
Utakapo anza kuzingatia sheria hii ya namba yako ya bahati na ambayo ni muhimu sana kwako utaanza kuona mabadiliko katika mambo yako binafsi na ya kibiashara.
Mabadiliko hayataonekana ghafla lakini utayaona ndani ya muda mfupi wa kuanzia miezi mitatu na kuendelea. Inategemea ni kiasi gani utazingatia mambo haya na jinsi unavyo ongeza nguvu ya namba yako ya bahati.
NAMBARI NA BAHATI NASIBU
Je ni watu wangapi kati yenu hucheza bahati nasibu? Pengine sisi wote katika nyakati tofauti huwa tunacheza bahati nasibu kwa wakati mmoja au mwengine. Uchezaji bahati nasibu wa aina yoyote umekuwa maarufu sana duniani kote kama vile Lotto, Bingo, Sweepstakes, Lotteries na Mashindano ya aina nyingi ikiwemo mpira wa miguu.
Baadhi ya watu wana bahati kubwa sana wanapocheza bahati nasibu na wengine hawana bahati kabisa. Kwa vile kuna aina nyingi za bahati nasibu watu wengine watakua na bahati katika mashindano ya Farasi au wengine wakawa na bahati kubwa katika mashindano ya mpira wa miguu (Football).
Ili kujua wewe kama unabahati katika bahati nasibu ipi, angalia tarehe yako ya kuzaliwa. Kwa mfano mtu aliyezaliwa tarehe 23 Mei atatawaliwa na namba ya bahati 5 kwa sababu (2+3=5) na atafanya vizuri kwa kufuatia mtiririko wa namba 5 katika maelezo yatakayo fuata.
Mwisho usichukulie kucheza bahati nasibu kama ndio msingi wa maisha labda uwe na pesa nyingi kupita kiasi ya kutumia na kupoteza.
Mtu wa number 1 A J S
Wale waliozaliwa tarehe 1, 10, 19 na 28 au mwezi wa nne au wa nane kawaida wanakua wcheza bahatinasibu wazuri katika biashara, matarajio au Mashindano. Mtu huyu wa namba 1 iwapo atajizuia na uzembe katika Matarajio yake basi huenda akapata bahati kubwa kwa mfululizo. Ambapo mashindano mengine ya mbio za aina yoyote anatakiwa aepukane nayo kama vile mashindano ya mbio za Farasi, Pikipiki, Magari. nk.
Mtu wa number 2 B K T
Wale waliozaliwa tarehe 2, 11, 20 na 29 au waliiozaliwa mwezi Mei au Julai watafanya vizuri wakibet kwa wanaotarajiwa kushinda yaani (favourites). Mashindano ya michezo ya baharini kama vile Yatch, mashindano ya kujaza maneno (Crossword) Mashindano ya Spelling na mashindano ya Bingo hizi ndizo sehemu ambazo Mtu huyu wa namba 2 anaweza kufanya vizuri katika bahatinasibu lakini wawe na subira sana na wawe makini.
Mtu wa number 3 C L U
Wale waliozaliwa tarehe 3, 12, 21 na 30 au waliozaliwa mwezi wa Machi na Desemba ki sheria ya nambari huwa ni watu wazuri sana katika kucheza bahatinasibu hasa katika mashindano ya mitindo, mbio za Farasi, mbio za mitumbwi (Yatch), Tennis, Golf kwa sababu mtu wa namba 3 huwa anajigamba sana kwa yale wanayoyafanya katika michezo ya bahatinasibu
Mtu wa number 4 D M V
Wale waliozaliwa tarehe 4,13, 22, 31 au waliozaliwa katika miezi Februari au Agosti hawa huwa hawana bahati sana katika kucheza bahatinasibu ya aina yoyote. Ikiwa mtu huyu wa namba 4 ni lazima acheze bahatinasibu basi wale washindani wasiofikiriwa kushinda ndio chaguo lao zuri kuweka pesa zao. Aidha mashindano ya kutumia mashine iwe ndio chaguo lao.
Katika namba zote Mtu huyu wa namba 4 asitegemee kuishi katika kucheza bahati nasibu ftgd pekee.
Mtu wa number 5 E N W
Wale waliozaliwa tarehe 5, 6 v14, 25 au katika miezi ya Juni na Septemba kawaida huwa nabahati nzuri sana kuliko namba zozote, hasa wale waliozaliwa tarehe 23 ya mwezi wowote. Mbio za aina yoyote, Roulette wheel, Dice, Karata na michezo yote ya aina hii. Michezo yote hii inakuja chini nguvu ya namba 5.
Lakini vile vile mtu huyu wa namba 5 lazima ajizuie na kuwa mzoefu sana wa kucheza bahati nasibu kwani watu hawa kawaida hupenda sana kujaribu.
Mtu wa number 6 F O X
Wale waliozaliwa tarehe 6, 15, 24 au wale waliozaliwa katika miezi ya Mei na Oktoba hufanya vizuri katika mashindano yote ya Ardhini kama vile mbio za farasi, mbio za Mbwa, mbio za binadamu na mashindano kama hayo. Mtu wa namba 6 kama vile Mtu wa namba 5 huchukuliwa ni mtu mwenye bahati sana katika kucheza bahati nasibu, lakini unapoanza kukosea basi acha kucheza mara moja.
Mtu wa number 7 G P Y
Wale waliozaliwa tarehe 7, 16, 25 au wale waliozaliwa katika miezi ya Machi na Julai lazima wawe mkini sana iwapo ni lazima acheze bahatinasibu. Chagua wanaotaragiwa kushinda. Kawaida ya namba 7 sio kutarajia jambo lakini ni kutafuta ukweli wa ndani na busara. Mashindano ya kutumia akili sana kama vile Crosswords, hesabu au mashindano ya kisayansi na mashindano kama hayo huleta mafanikio makubwa kwa watu wa namba 7
Mtu wa number 8 H Q Z
Wale waliozaliwa tarehe 8, 17, 26 au waliozaliwa katika miezi ya Januari na Oktoba ki sheria ya nambari wanatakiwa wasicheze bahatinasibu kabisa.. Kazi ngumu na kujituma kawaida huwa ni mchezo wa maisha (Game of Life) kwao. Lakini ikiwa ni lazima ucheze bahatinasibu basi ujue ushindi ni mdogo sana na chagua mashinda ya Ardhini kama vile Mpira wa Miguu, Mashindano ya Farasi au Ndondi. Bahati nasibu Nzuri kwako ni kuhifadhi pesa zako zote utakazoweza.
Mtu wa number 9 I R
Wale waliozaliwa tarehe 9, 18, 27 au katika miezi ya Aprili na Novemba hufanya vizuri katika mashindano yenye ushindano mkali kama vile Mieleka (Wrestling) Mpira wa miguu, kupiganisha Jogoo, Vita vya Fahali (Bull Fight) karata, Roulette na michezo ya uwanjani, hata kama mtu huyu wa namba 9 atakosea kidogo hurekebisha kwa kushinda.

Post a Comment

0 Comments