Karibu ndugu msomaji katika mada hii muhimu.
Haraka haraka unapoliona tangazo la Schorlaship,unajisikiaje? Je, umekata tamaa ya kupata schorlaships? Pengine bado unayo nafasi ya kupata scholarship, endapo utazingatia mambo ya msingi. Makala inadokeza mambo hayo ya msingi.
1. Kupata nafasi ya chuo : Ni wazi kuwa unataka schorlaship (uhisani) ili kusoma katika chuo fulani, basi ni muhimu kwanza uwe umepata chuo. Unahitaji kupata chuo kwa sababu kuu zifuatazo:
- Kwanza mhisani unayetegemea akufadhili ni muhimu kwake awe na uhakika kuwa unakidhi viwango vya kusoma kozi fulani, na kuthibitisha hivyo, ndio maana umeweza kukubaliwa kujiunga na chuo husika.
- Pili, unapokuwa umekubaliwa katika chuo fulani maana yake utapokea maelekezo ya gharama zote za masomo yako chuoni hapo, na pia itakuwa rahisi kwa mhisani kuwa na uhakika wa gharama unazomtajia.
- Tatu , wahisani wengi hutoa ufadhili moja kwa moja kupitia vyuo, hivyo unapokuwa umepata kukubaliwa na chuo fulani, basi ni rahisi kuomba ufadhili toka kwa wahisani wanaofadhili kupitia chuo husika ulichokubaliwa. Mfano: MASTER SCHORLASHIP IN SWEDEN
2. Maandalizi kabla ya kuaply:
- Hakikisha una matokeo mazuri ya darasani: Wahisani wanataka kuwa na uhakika kuwa utaweza kuhitimu masomo watakayokufadhili, hivyo basi matokeo yako mazuri ya darasani kabla ya ufadhili wako, ni dalili nzuri kuwa unao uwezo wa kuenda kusoma na kufanikiwa kumaliza hivyo, fedha za wahisani hazitopotea bure. Baadhi ya wahisani huenda mbali zaidi kwa kutaka kufahamu kuwa elimu watakayokupatia itakuwa kweli ya manufaa kwako na kwa jamii hivyo hupenda kupata maelezo toka kwako namna ambavyo utaitumia elimu utakayopata. Ndio maana maombi yako ya ufadhili mara nyingi huambatana na barua ya. kujitambulisha na kujieleza malengo yako kuhusiana na fani unayoenda kuisomea.
- Hakikisha lugha hususani kiingereza , Kichina au Kijerumani kinapanda vema:Nimetaja hapo juu, kuwa kuna kujieleza kuhusu fani unayoenda kusoma inavyoendana na malengo yako na manufaa kwa jamii kwa ujumla. Utaweza kujieleza vema kupitia lugha sanasana huwa ni kingereza
- Boresha uwezo wako wa mawasiliano: Utahitaji kuandika barua na wakati mwingine hata kuhudhuria usaili wa ana kwa ana na wahisani, hivyo uwezo wako wa kufanya mawasiliano fasaha ni muhimu. Jizoeshe kufuata kanuni za mawasiliano fasaha. Rudia tena kusoma Communication Skills.
3. Wakati wa kuapply
- Soma maelekezo vema: Amini usiamini, kila elekezo lililowekwa katika tangazo la schorlaship lina kusudio lake maalum, hivyo basi hakikisha unasoma maelekezo yote, na tena kwa ufasaha. Hii inajumuisha, kusoma mambo kama vile lini mwisho wa kuapply, mambo gani unatakiwa kueleza katika barua ya maombi, nyaraka unazotakiwa kuambatanisha wakati wa kutuma maombi, jinsi ya kutuma maombi n.k.
- Fuata Maelekezo kwa usahihi: Kusoma tuu maelekezo haitoshi, bali unatakiwa uyafuate vema.
4. Nini cha kutarajia kuhusu Schorlaships
- Gharama zitakazolipiwa:Tambua pia inawezekana kabisa wahisani wasifadhili kila aina ya gharama za masomo yako. Hivyo unaweza kuendelea kutafuta wahisani wengine zaidi ili kupata ufadhili wa kutosha kulipia gharama zako. Mara nyingi huwa ni full , nikiwa na maana watakulipia kila kitu lakini nimuhimu kufahamu kuwa usiwaze tuu kupata mfadhili mmoja , angalia uwezekano wa ufadhili mwingine, na pia wewe mwenyewe namna unavyoweza kujilipia
Unaweza kusoma hapa masharti ya kuomba sscholarship za Confucius institute ya China
Bofya>> hapa>>
Njia ambazo utaweza kuzipata scholarship Mbali Mbali zinazo tangazwa ni kwakupitia Google, unaweza kutafuta kwa lugha ya kingereza, kisha kuchagua inayo endana na wewe! Mfano Mimi napenda maswala ya lugha basi nitatafuta language scholarship nk.
Mwandishi Wa makala haya ni mtaalamu Wa uandishi masuala ya lugha, kiswahili&Tehama na Sanaa.
info.masshele@gmail.com
0 Comments