Alifika eneo hilo akiwa amepakizwa kwenye toroli akisukumwa na mjukuu wake
Amuria,Uganda. Mzee wa miaka 85 amefariki dunia akiwa amepanga foleni ya kupata fedha za uzeeni zinazotolewa na mpango wa Usaidizi wa Jamii kwa Uwezeshaji (Sage) katika Wilaya ya Amuria.
Mzee huyo aliyefikishwa eneo hilo akiwa amepakizwa kwenye toroli alifahamka kwa jina la Hennrick Olinga alifariki katika kaunti ya Aberillela akisubiria kupata huduma hiyo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi msaidizi wa Kaunti ya Amuria Simon Peter, tukio hilo lilitokea saa kumi jioni wakati yeye akiwa kwenye kikao.
“Ilitulazimu kufunga zoezi hili na kuanza kushughulikia mwili wa marehemu tukauchukua na kuusafirisha kijiji kwake cha Awajakitoi,” amesema.
Wananchi wengi wanaokaa maeneo hayo imedaiwa kwamba wanaishi katika mazingira magumu, hususan wazee ndio maana wanapatiwa fedha za kujikimu za uzeeni.
Desemba 2016, mzee mwingine wa umri wa miaka 88 alipoteza maisha baada ya kupokea fedha zake za miezi miwili Sh50,000 eneo hilo.

0 Comments