Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Simba, AS Vita vitani kwa Tusiyenge




ACHANA na habari ambazo zinazagaa mitandaoni kuwa Klabu ya AS Vita ya DR Congo, imemsajili mchezaji wa Gor Mahia ya Kenya, Jacques Tusiyenge, ukweli ni kwamba mchezaji huyo tayari yupo katika orodha ya nyota wanaowaniwa na Simba.
Japo AS Vita ipo tayari kumsajili mchezaji huyo kwa gharama yoyote, lakini Simba wameonekana kuwa ‘siriasi’ zaidi, wakijipanga kuvunja benki kwa ajili ya mkali huyo.
Akizungumza  jana, Meneja wa mchezaji huyo, Mnyarwanda Patrick Kagunga, alisema kuwa Simba ndio walikuwa wa kwanza kutuma barua ya kumhitaji mchezaji huyo, ila atakayefanikiwa kumtwaa ni yule atakayekuwa na dau kubwa zaidi.
“Tusiyenge ni mchezaji ambaye ana uwezo mkubwa sana na timu nyingi zimeshanieleza zinamhitaji, lakini kwa upande wa Simba na AS Vita, wao ndio wanauhitaji mkubwa zaidi na mara kwa mara wamekuwa wakinipigia simu.
“Ninachoangalia ni fedha, hata wao wanamhitaji ili akawaingizie fedha, hivyo atakayefanikiwa kutoa dau kubwa zaidi hakuna shida, atamchukua kwa sababu mpira ndio kazi yake kokote anaweza kwenda,” alisema Kagunga.
Katika kikosi cha Simba, wachezaji waliopo chini ya meneja huyo ni Meddie Kagere, Adam Salamba na Deogratus Munishi ‘Dida’.

Post a Comment

0 Comments