1.0 Utangulizi,
Katiika
kazi hii tutaangalia mi singi ya
ulinganishaji katika kazi za fasihi ambapo kazi za kifasihi ya Kiswahili
na fashihi ya Kimagharibi zitatumika
kama mifano. Majibu ya swali hili yamegawwa katika sehemu tatu. Sehemu
ya kwanza ni utangulizi ambayo inahusu fasili ya fasihi linganishi, sehemu ya
pili ni kiini cha swali na mwisho ni hitimisho.
Wellek
na Warren (1948), wamefasili dhana ya fasihi linganishi kuwa ni mbinu itumiwayo
na wahakiki wengi wakazi ya fasihi hata wasayansi kwakujadili njia maalumu ya
usomaji wa sanaa mbalimbali ulimwenguni. Ulinganishi unaweza kuwa wa fasihi ya
kiafrika na Kizungu ama fasili ya kizungu dhidi ya Kihindi. Ulinganishi unahusu
ulinganishaji wa kazi za mataifa mbalimbali na sio za kitaifa peke yake.
Vilevile
Henry Remark (1971) anafasili fasihi linganishi kama uwanja wa kifasihi unao
husika na uchanganuzi na mahusiano ya kifasihi, nje ya mipaka ya nchi moja na
fani nyinginezo.
Kwaujumla,
fasihi linganishi ni ulinganishi wa kazi za kifasihi baina ya mwandishi
mwenyewe, mwandishi na na mwandishi mwingine, jamii na jamii au taifa na taifa.
2.0 Misingi ya ulinganishaji.
Hiininguzonamiongozoimwongozayomlinganishajikulinganishakazimbalimbali
za kifasihi, na humwezesha mlinganishaji kushughulikia kipengele kimoja baada
ya kingine wakati wa shughuli ya ulinganishaji. Katika kazi hii tutamakinikia
misingi mitano kama ifuatavyo;
2.1 Dhamira
Katika
kipengele hiki mwandishi hujikita katika kuangalia kuingiliana na kutofautiana
kati ya dhamirazakazimbilitofautizakifasihi. Kwa kutumia msingi huu katika
kulinganisha fasiihi za Kiswahili na Kimagharibi, dhamira mbalimbali zinafana
ingawa kazi hizozinztoka katika Mabara
tofauti yenye wakaaji wanaotofautiana. Mfano
suala la umasikini linavyo jadiliwa katika riwaya
ya usiku utakapo kwisha, ambapo tunaona marafiki wawili Gonza na Chioko
ambao walikuwa ni masikini na walisaidina vivyo hivyo katika Hekaya
za Pinokio swala hili la umasikini
limejitokeza na mafundi wawili masikini
ambaoni Cillegia na Geppetto, walikuwa
wakisaidiana. Vilevile masuala ya udanganyifu
yanayojitokeza katika Hadithi za Esopo ambapo Beberu alidanganywa na Mbweha akatumbukia
kisimani ,swala hili la udanganyifu linajitokeza pia katika tamthiliya ya Ngoswe Penzi kitovu cha uzembe ambapo Mazoea alidanganywa. Katika kutofautiana kwa kazi hizi kidhamira
ni kuwa fasihi za kimagharibi hazizungumzii maswala ya uganga na uchawi.
2.2
Historia
Ni
taaluma inayohusu matukio ya mbalimbali ya kipindi kilichopita na wakati
ujao.Historia inasaidia kulinganisha kazi za fasihi za mtunzi mmoja au wawili
zilizoandikwa katika vipindi viwili tofauti na kuona mtagusano au muachano wa
kazi hizo kihistoria. Kwa mfano: Katika ulinganishi wa kazi za zamani za
Kezilahabi na kazi za hivi karibuni kama kuna kufanana au kutofautiana kwa kazi
hizo. Kipengele cha kihistoria humsaidia mwanafasihi linganishi kujua kazi ya
kipindi fulani cha kihistoria na kazi nyingine ya kipindi kingine ili kutambua
kama kazi hiyo hiyo imejirudia au inautofauti. Mfano Tamthiliya ya Mfalme Edipode ya karne ya 5 na Utenzi
wa Nyakiiru ya karne ya 19 kuna matukio ya kihistoria yamejirudia, kujirudia
huko huhusisha wakati. Mlinganishi wa kazi za fasihi kwakutumia historia
anaweza kubaini ujirudiaji wa kazi ya kifasihi katika vipindi tofauti vya
kihistoria.
2.3 Itikadi,
katikakulinganishakaziza
kifasihi, suala la itikadi huweza kufanana au kutofautiana kutoka kwa mwandishi
mmoja hadi mwingine, mathalani katika kufanana kiitikadi kwa kazi za kifasihi
na kimagharibi kuna itakadi za kimapinduzi ambapo wanaamini kwamba tabia njema
ndio husababisha ujenzi wa jamii mpya. Mfano Shaban Robert
huwatakawatuwawenamaadilihivyohivyoukimuangaliamwandishiwaHekayazaPinikioanawaonyawatoto dhidi ya tabia ya kusema uongo kwa
kumtumia mhusika Pinoko ambaye pua yake alikuwa ndefu kila anapodanganya.
2.4 Utamaduni
Utamaduni
ni jumla ya mtu au jamii inavyoishi na kujiwekea miongozo itakayo iongoza jamii
hiyo, mwanajamii analo jukumu la
kuifuata misingi hiyo. Katika
ulinganishaji wa kazi za kifasihi ya Kiswahili na Kimagharibi, msingi
huu humwongoza mlinganishaji katika kunga’amua ikiwa kazi hizi kutokakatikajamiitofautizinafananakitamaduniama
laa, Aidha katika ulinganishaji wa kazi hizi tunaona kuingiliana kwa vipengele vya kiutamaduni wa
jamii moja na jamii nyingine, mathalani katika jamii za Waswahili suala la
kuoana kwa watu wenye nasaba moja ni kosa ambapo suala hili linaonekana pia
kufanana na jamii ya watu wa magharibi hususani Ugiriki ambao nao ni kosa
kuoana kwa watu wa nasaba moja. Mfano katika tamthiliya ya Mfalme Edipodena Tamthiliya ya kwenye
Ukingo wa Thim. Vilevileutamaduniwakuchezangomakatika vikundi unaojitokeza
muongonimwakazinyingizakiswahilikamaNgomayaMwanamalundi,katikafasihizaKimagharibini
tofauti kwani wao hucheza muziki katika shoo na maonesho
mbalimbali kama ijitokezavyokatikahadithizaEsopokatikakisacha Nyaninawacheza shoo.
2.5 Falsafa ;
Sodipo
(1973) anafasili falsafa nimawazo, fikra na udadisi kuhusudhana na kanuni
zinazotusaidiakuongeza uzoefu kuhusu maadili dini, siasa ,sheria ,
saikolojia,historianasayansiyajamii. Katika
ulinganishaji wa kazi za Kiswahili na zile za Kimagharibi kuna
kuhitilafiana na kutaguzana katika kipengele hiki ambapo katika kufanana
kifalsafa baina ya waandishi wa kazi hizo suala la falsaya ya Euprase Kezilahabi
ya “ kifo sio mwisho wa kuwako” inajitokeza pia katika kazi ya hekaya za Pinokio ya Mtaliano
Carlo Collodi. Aidha katika kutofautiana kifalsafa baina ya kazi za Kiswahili na kimagharibi ni
katika falsafa ya wema kuushinda ubaya inayopatikana katika kazi za Kiswahili
zilizoandikwa na Shaaban Robert na falsafa ya Ubaya kwa ubaya inayopatikana
katika kazi ya Wagiriki Pinkey na Aesopus
walioandika hadithi za Esopo katika kisa cha Nyoka na Nyigu.
3.0 Hitimisho
KwaUjumlakwabaadhi
ya vipengele kazi za kifasihi za Kiswahili na zile za kimagharibi
zinafanana nakuitofautiana kwa uchache
katiika baadhi ya vipengele.
MAREJELEO
Aesopus
(1698). "Fabularum Aesopicarum
Delectus". google.co.uk.
Collodi
C, (1883) Le adventure di Pinocchio, Firenze.
Italy
Sodipo
(1973), Woman and African Society.
France: Strasbourg
Remark,
H. H. (1971), Comparative Literature:
Its Definition and Function. Southern Ilions
Carbondale.
Wellek, R . na Warren, A. (1948), Theory
of Literature. Horcourt, Brace and Company: New
York.

0 Comments