Na E. Mashele
info.masshele@gmail.com
Prufu ni mswada uliosetiwa kwenye sura ya kuwa kitabu. Hii ikiwa na maana kitabu huwa kati ya kuhaririwa na kuchapwa.
prufu huweza kuwa katika muundo wa A4 au B5 hadi 6, kulingana na usanifu wa kitabu na walengwa wa kitabu.
Je kunatofauti kati ya kusahihisha prufu na Uhariri? Ndio tofauti zipo nyingi sana ukizingatia uhariri ndio huanza kwanza ndipo kusahihisha prufu hufuatia. Lengo kuu la kusoma Prufu ni kusahihisha makosa mbalimbali yaliyo sahaulika wakati wa uhariri.
Je kusahihisha prufu ni muhimu? , usomaji wa prufu, ni muhimu sana kwani ni hatua ya mwisho ya upitishaji wa mswada kabla ya kuingizwa mtamboni.
Msahishaji wa prufu anapaswa kuwa na 1. Jicho la kiuhariri
2. Stadi na mbinu
3. Vifaa mbalimbali.
Muhimu , usomaji wa prufu ni kama ule wa mtoto mdogo anaye jifunaza kusoma.
0 Comments