![]() |
| Prof, Aldin .k. Mutembei Picha na mtandao. |
Profesa Aldin .K. Mutembei alipata shahada ya Udaktari kutoka chuo kikuu cha Leiden na baadaye mwaka 2015 kutunukiwa uprofesa katika chuo kikuu cha Dar es salaam: mkufunzi huyu wa fasihi na lugha Amewahi kuwa mkurugenzi wa taasisi ya taaluma za kiswahili, na sasa ni mkuu wa kigoda cha Mwalimu nyerere na mkurugenzi katika taasisi ya lugha na utamaduni ya conficuous.
Pamoja na kuandika na kushughulikia mambo mbali mbali ya kifasihi, Kuanzisha nadharia mpya ya uchambuzi wa fasihi iitwayo "Korasi katika fasihi ndiyo iliyompaisha zaidi, kwani imekuwa miongoni mwa nadharia mpya inayotumika kuhakiki kazi za kifasihi na yeye akitambulika duniani kama muasisi wa nadharia hiyo.
MAELEZO KUHUSU MKABALA WAKE
Mkabala Wa Ki-Korasi Katika Kuchambua Kazi Za Fasihi Ya KISWAHILI
"Kwa wachambuzi na wahakiki wa fasihi ya Kiswahili, mtazamo umekuwa ni wa kugawa makundi mawili: fani na maudhui. Hata hivyo, karibu wote wanakubaliana kuwa mgawanyo huu ni wa kinadharia zaidi na unafanyika kwa ajili ya uchambuzi na uhakiki; kwani katika hali halisi maudhui huwezi kuyatenga kutoka katika fani (Senkoro 1982). Ingawa hivi ndivyo inavyojulikana, hakuna aliyeweza kupendekeza njia ya uchambuzi itakayoziweka pamoja dhana za maudhui na fani. Kwangu mimi, tatizo liko katika umapokeo, na kwa hiyo wachambuzi na wahakiki ambao bado wanashikilia dhana za fani na maudhui kwamba ndizo pekee zitumikazo katika uchambuzi wa fasihi wamegubikwa na mazoea ya kimapokeo ambayo mara nyingi hugomea mabadiliko. Dhana za fani na maudhui zimesimama kama sheria-mama katika uchambuzi na uhakiki wa fasihi. Kutokana na mtazamo huu wa ki-fani na ki-maudhui , wahakiki na wachambuzi wa fasihi kama vile tamthilia wameweka vigezo ambavyo havina budi vifuatwe iwapo mtu atataka kuichambua na kuihakiki kazi ya fasihi. Vigezo hivi sasa vimechukuliwa kama ni sheria katika uchambuzi na uhakiki wa tamthilia. Hata kuna waliothubutu kuweka "sheria" katika ubunifu wa kazi za fasihi Lakini uchambuzi, na hata uhakiki, kama ulivyo utunzi wa kifasihi, ni vigumu kuubana kwa sheria kama hizo. Suala la sheria katika usanii linaelekea kuwa jadi ya wanamapokeo (Abedi 1954; Mayoka 1984). Jambo hili limepingwa vikali katika usanii wa ushairi wa Kiswahili (Kezilahabi 1974; Mulokozi na Kahigi 1979). Likapingwa na E. Hussein kuhusu tamthilia aliposema: "Kuandika mchezo wa kuigiza ni kuumba sanaa. Na sanaa hukataa maelezo; kamwe haitaki sheria" (Hussein 1983: 195). Katika makala haya linapingwa katika uchambuzi wa fasihi ya Kiswahili. Nasisitiza kuwa fani na maudhui zisichukuliwe kuwa ndio dhana pekee zinapopaswa kuangaliwa wakati wa kuchambua fasihi. Dhana ya korasi ikieleweka vizuri, itaonekana kuwa ni kipengele kinachopaswa kuangaliwa kwa upekee wake na kikatumika katika uchambuzi wa kazi ya fasihi"
Licha ya kushughulikia kipengele hicho muhimu cha uhakiki, prof Mutembei mpaka sasa ameshughulikia maswala mengine ya fasihi ya kiswahili kama vile fasihi ya kiswahili na Ukimwi, fasihi ya kiswahili na teknolojia, fasihi linganishi na masuala mengine ikiwemo uandishi wa ushairi.
Pamoja na hayo Profesa Mutembei amekuwa akiipigia debe fasihi ya kiswahili na lugha ya kiswahili. Mwaka 2014, kituo cha habari za kiswahili katika mtandao wake wa kijamii kilimtaja kama Wole Soyinka wa Afrika mashariki. Aidha amekuwa mstari wa mbele katika mijadala inayohusu lugha ya kiswahili na fasihi ya kiswahili kiujumla.
Unaharakati wake kwa lugha ya kiswahili
Mutembei ni mmoja kati ya wataalamu wanaoamini itakuwa siku moja lugha ya kiswahili kuwa lugha ya bara zima la Afrika huku akishauri lugha zote za kiafrika kuchangia kukijenga kiswahili, Mara kadhaa amekuwa akilikazia hilo katika mjadala wa kiswahili kinawenyewe na Mohammed Khelef katika Dw.
Mutembei ni mmoja kati ya wataalamu wanaoamini itakuwa siku moja lugha ya kiswahili kuwa lugha ya bara zima la Afrika huku akishauri lugha zote za kiafrika kuchangia kukijenga kiswahili, Mara kadhaa amekuwa akilikazia hilo katika mjadala wa kiswahili kinawenyewe na Mohammed Khelef katika Dw.
![]() |
| Aldin Mutembei, picha na mtandao Unaweza kusikiliza moja ya mijadala aliyoshiriki katika kituo cha Dw kiswahili kuhusu kiswahili kuwa lugha ya afrika katika kiswahili kina yenyewe. Hapa |
Je Kwa hayo yote anastahili kuwa ndiye nguli wa fasihi ya kiswahili kwa miaka hii? Angalizo, katika kujibu swali hili lazima uzingatie kuwa mtaalamu huyu hajajikita sana katika kuandaa kazi za kifasihi Bali kuchambua, kueleza namna ya kuzichambua, kuziainisha, na kuzilinganisha kwa ajili ya msomaji.
Miongoni mwa machapisho yake pamoja na yale aliyoshiriki.


0 Comments