Taarifa kutoka Dodoma zinaeleza kuwa treni ya abiria imeanguka na kusababisha vifo na baadhi ya watu kujeruhiwa.Idadi ya waliokufa au kujeruhiwa bado haijatolewa na mamlaka husika.
Mwandishi wetu aliyeko Dodoma anaeleza kuwa maiti na watu waliojeruhiwa wanasafirishwa kwenda hospitali ya mkoa kutoka eneo la ajali.
Treni hiyo ya reli ya kati ilikuwa safarini kutoka Dar Es Salaam kwenda bara. Tutaleta taarifa zaidi kadri zinavyopatikana.
Taarifa zaidi zinafuata...
0 Comments