MAANA
YA UTAFITI NA AINA KUU ZA UTAFITI
Utafiti ni nini?
Utafiti ni njia ya
kupatautatuzi wa swala fulani katika jamii na mazingira ya binadamu kwa njia ya
uchunguzi unaotumia nadharia za kitaaluma. Waaidha utafiti ni njia maalum inayofuatwa ili kufikia ujuzi au
taarifa muhimu inayokusudia kuchangia katika usomi wa kina na uchunguzi wenye
mweleko wa kimaantiki.
Utafiti wowote ule
hauwezi kufanyika wala haukamiliki pasi kuongozwa na nadharia kuanzia mwanzo
hadi mwisho.
Migao ya tafiti
Utafiti hugawika katika matapo
mbalimbali kwa kutegemea madhumuni na maksudi ya utafiti.
Uainishaji huu ni kama ufuatavyo:-
§ Uainishaji wa Tafiti
Kimakusudi
§ Uainishaji kwa kutumia
mbinu za uchanganuzi
§ Uainishaji Kulingana na
Aina za Utafiti.
1.
Utafiti wa kimaksudi
a.
Utafiti wa Kimsingi (Basic Research)
Hii ni aina ya utafiti ambao hutumiwa kujaliza ufahamu
ambao jamii au mtafiti hana kuhusu swala fulani katika jamii.Utafiti huu
hutumiwa katika kujaribu kujifunza mambo au vitu ambavyo kwa kawaida havikai
kuwa wazi au havionyeshi umuhimu wake mara moja.
Utafiti huu huelekezwa na ari kisha ukachochewa na hamu
ya kuongeza ujuzi na huusisha upataji wa ufahamu kuhusu jambo fulani. Lengo
lake kuu ni kujibu maswali ya kwa nini? Nini? Na vipi? Kakika hali hiyo utafiti
huu huongeza hali ya mtafiti na yeyote kufahamu maswala nyeti na muhimu. Aghalabu
utafiti huu huwa hauna lengo la papo kwa hapo.
Utafiti kama huu
huangazia katika uzalishaji wa ujuzi wa kisayansi na kuukuza ujuzi huo
kutoka sehemu pana ili kutoa masuluhisho katika sehemu zinazilingana sehemu
hizo. Ifahamike kuwa utafiti huu hujulisha
na kuongeza ujuzi katika nyanda za elimu au usomi.\ Vile vile aina hii ya
utafiti huzalisha ujuzi mpya ambao ujuzi huu hutumiwa katika uboreshaji na
upanuzi wa nadharia zilizotangulia.Ifahamike kuwa utafiti aina hii ndio unaofanywa na wasomi ili kujipatia shahada za
uzamili, uzamifu n.k.
Mifano ya utafiti wa kimsingi
Wakati rununu
zilipokuja au kugunduliwa, wanasayansi na watafiti mbalimbali walikuwa na hofu
kuhusu matumizi ya kifaa hicho cha mawasiliano wakiendesha gari.wao walionelea
kuwa kungekuwa na ongezeko la ajali barabarani. Hofu yao haikuwa kwamba eti
madereva wataendesha magari kwa mkono mmoja huku wakiwasiliana kwa simu bali
ni kwa sababu ya uzingativu
unaohitajika wakati wa kuongea kwa simu. Makisio yao haya yalitokana na
nadharia za kimsingi kwa kwa kutozipa kipaumbele.
Mifano zaidi ya utafiti wa kimsingi.
Ugunduzi wa miale
ya uyoka(X-rays) ambayo katika uchunguzi wa kasoro kwenye mifupa. Utambuzi wa kropromazini(chropromazine), dawa
ambayo hutumiwa katika matibabu ya
sizofrenia(schizophrenia)
Utambuzi wa
mawiano ya giza ambayo yalisaidia katika maendelezi na makuzi ya nadharia ya
kimsingi ya kisayansi kuhusu hali ya
kuona ambayo ilesaidia kupata suluhu ya kutibu maginjwa ya macho yanayoambatana
na upofu wa giza na kusoma mialeya uyoka.
Utafiti wa
kisaikolojia kuhusu kufanya maamuzi ambayo yalikuwa nguzo katika nyanda za
elimu, utabibu and uchumi.
Matokeo ya kisaikolojia kama inavyojitokeza katika
mifumo mbalimbali ya kisheria: utathmini wa ushahidi, ushahidi wakati wa
matokeo mbalimbali n.k
b.
Utafiti Tumikizi (Applied Research)
Utafiti tumikizi hutafiti kuhusu swala maalum
na kutambua ikiwa nadharia fulani inatimiza matakwa yake au la.
Hivyo basi utafiti tumikizi hutumiwa data
moja kwa moja ili kutoa suluhisho kuhusu tatizo lililopo wakati uo huo.
Katika
utafiti huu, lengo ni kusuluhishaswala
lililopo katika mazingira husika wakati uo huo. “Keth Stanvich
mwanasayansi na mwandishi wa kitabu , To
Think Straight About Psychology(2007, ukursa 106)
Kielimu utafiti huu hutumika kubaini ikiwa
mbinu fulani zinazotumika zimefaulu au la. Kwa mfano ,matokeo duni ya mtihani wa Kitaifa(KCPE) katika shuleza
serikali nchini yameathiriwa vibaya sana na mfumo wa elimu bila malipo.
c. Utafiti Kiutendaji (Action Research)
Ni aina ya utafiti ambao kwamba
hufanywa na wale ambao wana nia na lengo la kuchukua hatua katika kusuluhisha
jambo fulani katika jamii. Jambo au tatizo hili huwa lile ambalo limeibuka na
limeikumba jamii wakati maalum na utatuzi wake huhitajika papo kwa papo
wala si wakati mwingine.
Mifano ya utafiti wa aina hii:
Muziki na athari zake kwa wanafunzi
katika makuzi ya stadi za uandishi.
Sababu za ongezeko la visa vya
kunyofolewa sehemu nyeti kwa wanaume katika kaunti ya Nyeri.
Sababu za kiwango cha juu cha wanafunzi hasa wa kike kuachia masomo njiani katika
jamii za kuhamahama.
Eneo fulani kuathirika na mafuriko ya maji ili
kuweza kutafiti ili kupata suluhu la tatizo hilo.
Sababu za ongezeko la visa vya wajakazi kuwateka
nyara na kutoroka na watoto.
Sababu za ongezeko la wanaume kuwaua kinyama wake
au watoto wao katika jamii.
d. Utafiti wa Kutathmini
(Evaluation Research)
Utafiti wa aina hii hufanywa kwa lengo la kuthibitisha
iwapo yaliyotarajiwa ndiyo yaliyotimia. Hivyo basi, utafiti huu huwa wa utaratibu
fulani wa kukusanya data kisha kuichanganua data hiyo. Kwa mfano, utafiti wa
aina hii unaweza kufanywa kuthibitisha kama mpango wa elimu ya bure umefaulu au
la.
2.
Uainishaji kwa kutumia
mbinu za uchanganuzi
a) Utafiti wa kueleza (Descriptive Research)
Ni aina ya utafiti ambao unakusanya data ambayo data hiyo
itauwezesha utafiti huo kufanya majaribio au kuyajibu maswali yanayohusu mada
ya utafiti wakati ule. Huu ni utafiti ambao hueleza jinsi mambo yalivyo.
Utafiti wa aina hii haudhihirishi wazi ikiwa ni wa mfumo
wa utafiti wa kimaelezo au wa kiidadi bali huzama katika aina zote mbili wakati
wa kuichanganua data.
Hatua zake hufuatana hivi:
- Kuunda malengo ya utafiti:
Pasi kuwepo na lengo ni
muhalisana kufanya utafiti wowote. Hivyo basi mtafiti sharti awe na lengo la
kumwongoza kama dira katika ufanyaji wa utafiti wake.
- Kuandaa vifaa vya kukusanya data:
o
Hizi ni nyenzo muhimu katika swala zima la utafiti.
Ni sharti mtafiti aandae vifaa vya kukusanya data akiwa nyanjani.
o
Vifaa hivi vinaweza kuwa vya aina mbalimbali
kulingana na sehemu ya kijiografia, tamaduni za walengwa, umri aidha hali ya
anga.
Mifano ya vifaa vya ukusanyaji data.
o
Shajara
o
Kamera
o
Video
o
Vinasa-sauti
o
Simu n.k
- Kuchagua sampuli.
o
Mtafiti huichukua sehemu fulani kama kiwakilishi
cha eneo zima ambalo analiangazia katika utafiti wake.
o
Katika utambuzi wa sampuli, mtafiti huhitajika
kuwamakini sana kiasi kwamba kila pembe na viwango vya walengwa vinashirikishwa
kikamilifu.
- Kukusanya data.
o
Huu ndio uti wa mgongo katika utafiti. Ifikapo wakati
huu, mtafiti hustahili kuwa makini huku akizingatia miongozo iliyoratibiwa
pamoja na kuandamana sako kwa bako na nadharia lengwa.
o
Ifikapo tamati basi data hii inaweza kuhifadhiwa
katika vyombo mbalimbali vikiwemo vya kisasa vya kielektroniki.
- Kuchanganua data.
Katika sehemu hii,
mtafiti huongozwa na kuelekezwa kwa kina na nadharia lengwa. Ni kutokana na
uchanganuzi huu ambapo mapendekezo yanaweza kufanywa pamoja na kuona iwapo
utafiti huo umeweza kuyajibu maswali tarajiwa.
Kimsingi utafiti
wa kueleza hujibu swali la “kwa nini?” maswali ambayo yanaweza kujibika ni
kufanya utafiti kuhusu mada yafuatayo:-
Je, walimu wana msimamo na nafasi bora kuhusu matumizi ya
vipakatalishi katika shule za msingi nchini Kenya?
Mifano zaidi:
Ni mbinu zipi za motisha zisizoonekana wala kushikika ambazo zinatumika katika karne ya 21 kwenye sekta ya utalii nchini Kenya.
Je, ni athari zipizilizopo katika ulaji na matumizi ya chakula kwa wanafunzi wa chuo kikuu chaKenyatta njeya chuo hicho?
Je, tofauti zipiku zilizopo katika vuguvugu la utetezi wa haki za raia na shirika rasmi laserikali lenye shughuli hizo?
Uratibu mpya wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na shirika la HELB una madharayapi kwa wasomina yeyote aliye na ari ya kutaka kujiongezea masomo?
Je,kuanzishwa kwa kituo cha runinga katika chuo kikuu cha Kenyatta kuna athari zipi kwa wanafunzi?
Ubora wa Utafiti wa kueleza
Ufanisi wa kuchambua mada zisizo kukaguliwa na masuala.
Kunao ufanisi mkubwa wa kuchambua na kuchanganua masuala yasiyokadirika.
Kunao uwezekano mkubwa wa kuchunguzanna kutafiti jambo katika mazingira yake halisi bila kuyabadili.
Upo uwezekano na nafasi kubwa ya kuunganisha mbinu bora katika ukusanyaji wa data.
Matatizo ya Utafiti wa kueleza
Ni vigumu kutafiti wala kuthibitishwa suala la utafiti lisilokadirika kitakwimu.
Wingi wa utafiti wa kueleza aghalabu si rahisi kuurudia kutokana na mbinu au maumbile ya utafiti huo.
b) Utafiti Linganishi (Casual – Comparative Research)
Huu ni utafiti ambao hutumiwa katikaulinganishaji wa vigeu ukiwa na nia au lengo la kutaka kuonyesha sababu za jambo au hali kuwa jinsi ilivyo.Katika funya hayo, utafiti huu huvilinganisha vigeu pasi kuyaingilia matokeo yake.Kwa hivyo ni utafiti ambao hujaribu kulinganisha chanzo na matokeo ya haliau jambo.Sifa zakeHujaribu kubaini chanzo na madhara ya uhusiano kati ya vigeu tofauti.
Inahusisha ulinganishi wa vigeu.
Sampuli haziwezi kuchukuliwa au kuteuliwa bila kufuata utaratibu na kuhusishwa kwa makundi mawiliau zaidi.
Haiwezi kuendesha au kuelekeza vigeu ambavyo vinajitegemea.
Ina gharama ya chini.
Inachukua muda mrefu sana.
Mifano zaidi.Jinsi gani mahudhurio katika shule ya malezi yanaweza kuathiri ukomavu wa mtoto kijamii mwishoni mwa shule ya msingi?
Jinsi gani kuwa na mzazi wa kike anayefanya kazi ya kuajiririwa inavyoathiri mahudhurio ya mtoto shuleni?
Ni kwa nini wafafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta wa mfumo wa ODEL hawafanyi vizuri sana katika kozi ya AKS 100 ikiliganiswa na wenzao wa daima chuoni katika kozi iyo hiyo?
c)
Utafiti Wiani
(Correlation Research)
Kwa ujumla, utafiti
wiani ni
utafiti ambao unavigeu viwiliau zaidi kutoka katikasampuli moja. Hivyo
basi mtafiti huwa kwake anajaribu kutafiti iwapoupo uhusiano mabadiliko katika
vigeu hivyo.Kuwepoau kutokuwepo kwa uhusiano ndiyo dira ya utafiti waaina hii.
Kukosekana kwa uwiano
katika vigeu husika kutalazimisha utafiti huo kutamatika. Lau uhusiano
utakuwepo baina ya vigeu hivyo basi utafiti huu utazidi kupiga hatua ili
kutambua aina ya uhusiano ule na chanzo chake.
Kuna aina tatu za uwiano:
v uwiano chanya:
Katikaaina hii ya uwiano ni kuwa kuongezeka kwa kigeu kimoja husababisha ongezeko kwenye kigeu kingine. Hii inaashiria kuwa kupungua kwa kigeu kimoja vile vile hulazimisha kigeu kingine kupungua.Kwamfano:- kiwango cha pesa ailizo nazo mtu huenda zikauiana na idadi ya magari anayomiliki. Ama kiwango cha pesa za matumizi alizo nazo mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta huenda kikauiana na aina ya chakula anachoagiza kwenye ukumbi wa maakuli.
v
Uwiano hasi:
Katika uwiano huu,
ni kuwa ongezeko la kigeu kimoja husababisha kupungua kwa kigeu kingine.Kwa
mfano uboreshaji wa sekta ya elimu nchini unaweza kupunguza visa vya uhalifu
katika jamii.Ikumbukwe kuwa sio eti
ukosefu wa elimu katika nchi husababishi
uhalifu katika taifa husuka. Inaweza kuwa ukosefu wa elimu na uhalifu
vyotevimesababishwa na hali ya umaskini katika nchi.
v
Ukosefu wa uwiano:
Katika hali hii, hakuna uwiano wowote katika
vigeu vinavyoangaziwa. Kwa mfano, kati ya mabilionea, amani huenda ikakosa
kithibitika na pesa. Hiiina maana kuwa ongezeko la pesa haliwezi kusababisha
amani katika maisha ya mabilionea.
3 Uainishaji Kulingana na Aina za Utafiti.
v
Utafiti wa Kukagua (Survey Research)
Hii ni aina ya utafiti
ambapo mtafiti hukusanya data kutoka kwa makundi husika na ili kutambua
haliyake kwa wakati ule kwamujibi wa kigeu kimoja au zaidi.
Utafiti huu huhitaji
mtafiti akusanye ujumbe wa kutosha kutoka kwa sampuli.
Ujumbe huu unaweza
kukusanywa kwa njia ya maswali au hojaji ya moja kwa moja. Hojaji hizi zinaweza
kufanywa kwa watu ana kwa ana wakiwa nyumbani,shuleni au hata kazini.Wakati
mwingine hata maswali huweza kutumwa kwa njia pepe au kwa kutumia mbinu yoyote ile
watu wakayajibu ya kuyatuma yalikotoka kwa kutumia njiaiyohiyo.
Aina mbili za utafiti wa
kukagua
§
Maswali(Questionnaires)
Utafiti huu wa kukagua kwa kutumia maswali unaweza
kutendeka kwa njia ya mtandao ingawa matatizo huwenda yakawa kuwa kuyapata
majibu ya moja kwa moja ni ngumu sana.
Hii ni kwa sababu watu walengwa huyajibu maswali
kulingana na vile wana wakati wao wa kutosha. Hii hupelekea matokeo
kutoridhisha.
Aina nyingine ya maswali ni ile ambapo sampuli
huchukuliwa na kupewa maswali yaliyoratibiwa ili wayajibu papo kwa papo huku
wakielekezwana mtafiti.
Mfano mzuri unaweza kuwa utafiti kuhusu taka na athari
zake.katika utafiti huu, mtafiti anaweza kuyatoa maswali katika kila nyumba
yakajibiwa na kutumwa kwake ama akayangoja yajibiwe papo kwa papo.
§
Hojaji (interview)
Katika hojaji ni kuwa ni kuwa mtafiti hushikiana moja kwa
moja na sampuli teule katika kujaliza matakwa yake. Hojaji huchukua muda mrefu
kutimilika. Maswali yote huelekezwa na mtafiti. Ingawa mtafiti hastahili
kukuelekeza kwenye majibu anayoyatakakuhusu hojaji teule.
v Utafiti wa kihistoria (Historical
research.)
Huu utafiti unahusu
usomi unaohitajika katika kukusanya ujumbe/taarifa kutoka wakati uliopita.
Mtafiti hutafuta data ambayo tayari ipo. Umuhimu wa utafiti huu ni kufikia
uamuzi wa chanzo, athari au mfuatano wa mambo yaliyotukia hapo awali na kuona
jinsi hayo mambo yameathiri ya sasa na pengine yataathiri yajayo. Mifano ya
tafiti za aina hii ni kama:
- Historia ya
jamii ya watu fulani
- Historia ya
mashirika au taasisi za elimu
- Historia ya
vyama vya kisiasa
- Historia ya
kanisa
- Historia ya
tamaduni fulani katika jamii.
Utafiti huu
ni njia muhimu katika kutafiti, kutambua na kufahamu yale yote yaliyotokea
awali na kutambua athari za matukio hayo katika jamii.
Utafiti huu
wa kihistoria ni kuwa unampa mtafiti wazo kuhusu swala fulani na namna wazo
hilo lilivyokuwa hapo awali.
Udhaifu wa
utafiti huu ni kuwa ipo mipaka katika data itumiwayo kulingana na lengo
linalotarajiwa.
v
Utafiti wa Uchunzaji
(Observation Research)
Kwenye utafiti wa aina hii, jambo linachunguzwa kwa
kuliangalia tu. Utafiti huu hutoa taarifa ambayo haina hisia za kibinafsi kwa
sababu mtafiti huchunuguzana kuangalia hali katika mazingira yake halisi au ya
kawaida.
Kwa mfano, mtafiti akitaka kuchunguza nidhamu ya
wanafunzi katika shule fulani, atahitaji tu kutembelea ile shule na kukaa
mahali – fiche na achunguze au aangalie tabia na mienendo yao bila wao kujua.
Katika mazingira ya aina hii, ataweza kupata hali halisi ya wale wanafunzi na
kuandika ripoti isiyo na ubinafsi wowote.
Mbinu za
uchunguzaji.
1. Uchunguzaji
uliodhibitiwa
2. Uchunguzaji
halisia
3. Uchunguzaji
shirikishi
Uchunguzaji
uliodhibitiwa
Huu ni uchunguzaji ambapo huelekezwa ambao
aghalabu hufanywa kisaikolojia katika maabara
Mtafiti huamua mahali ambapo utafiti
utafanyikia, wakati gani,na kwa kutumia sampuli zipi na katika hali gani. Hapo
mtafiti hutumiwa mbinu iliyojaribiwa na kutambulika wazi.
Mihimili yake
1. Uchunguzi
huu ni rahisi kuigwa na kutumiwa na
wengine kwa kutumia utaratibu uliotengwa.
2. Data
iliyopatikana katika uchunguzi wa aina hii huwa rahisi sana kuichanganua kwa
kuwa huwa ya kiidadi (kihesabu)
3. Huwa
ni rahisi kufanyika kwa muda mfupi.
Udhaifu wake
Uchunguzi huu unaweza kukosa uhalali kwa kuwa mtafiti huwa na dhana kuwa
amesimamiwa anapofanya utafiti hivyo basi huenda akatafiti visivyo kwa kuwa
katika hofu.
Huu ni utafiti ambapo sampuli huchunguzwa ikiwa katika mazingira yake ya asili. Katika hali kama hii mtafiti huhakikisha kuwa kuwepo kwake hakutaathiri ukusanyaji wa data kutokakwenye sampuli lengwa.
Mihimili yake.
·
Kwa
kuwa utafiti huu huchunguza tabia katika mazingira yake ya kiasili basi matokeo
yake huweza kutoa taswira kamili ya kile kinacholengwa baada ya uchanganuzi wa
data iliyokusanywa.
·
Huweza
kuibua ujuzi mpya kwa kuwa humpa mtafiti nafasi ya kutafiti hoja kwa ukamilifu.
Udhaifu wake
·
Utafiti
huu hufanywa kwa kuangaziwa sampuli ndogo sana hivyo basi huenda hili
likaathiri matarajio ya utafiti huo.
·
Ni
muhali kwa mtafiti mwengine kurudia utafiti huo kwa kufuata mbinu zilizotumika
na mtafiti aliyetangulia.
·
Mtafiti
vile vile anahitaji kupata mafunzo ya kutosha ili kuweza kutambua hali ambayo
huenda ikahitaji mbinu ya kisaikolojia katika utafiti.
·
Ni
muhali ni kubadili vigeu kwa vyovyote vile.
Uchunguzaji shirikishi
Katika aina hii ya
uchunguzi, mtafiti huungana au hujumuika na kikundi ambacho anahitaji
kukifanyia utafiti. Hivyo basi mtafiti
anachukua nafasi sawana jamii lengwa ambayo angeitafiti kwa kushiriki kikamilifu
sawa kama wao.
Katika aina hii
mtafiti vile vile anaweza kujibanza mahali kisha akaanza kuchunguza kwa umbali
pasi kujulikana wazi na walengwa kwa kila hatua.
Udhaifu wake
a.
Kuna uwezo wa
kukosekana kwa usiri wakati wa kutosha kwa mtafiti katika aina hii ya utafiti.
b. Iwapo mtafiti atajiingiza sana katika kikundi
anachokitafiti, upo uwezekano wa kupotea kwa Malengo au kuwepo kwa upendeleo.
Marejeleo
Ethridge,
D.E. (2004) “Research Methodology in Applied Economics” John Wiley & Sons,
p.24
Fox, W.
& Bayat, M.S. (2007) “A Guide to Managing Research” Juta Publications, p.45
Quinn,P.M.(1990).Qualitative
Evaluation and Research Methods.
Nsubuga,
EHK (2000)Fundamentals of Educational Research.
Mugenda, O. na Mugenda A.M., (1999). Research Methods. Nairobi: ACTS Press.
Prewit, K. (1974). Research Methods. IDS, University of Nairobi.
Lokeshi (1984). Methodology of Educational Research.
Kasomo Daniel, 2006. Research Methods in Humanities and
Education. Egerton University Press
Nyandemo, S.M. (2007) Research Methodology, Methods and
Approaches, Richmonds Designers and Printers.
Gatara, T.H. (2010) Introduction to Research
Methodology. The Olive
Marketing and Publishing Company.
Mishra, R.C. (2005) Encyclopedia of Educational
Research, A.P.H. Publishing Corporation, New Delhi.
0 Comments